Ilikuwa ni kazi ambayo nilijua kabisa rafiki yangu Joyce angeweza
kuifanya, moja kwa moja nilimpigia simu na kumjulisha ili aweze kupeleka
vyeti vyake. Ni muda mrefu Joyce alikuwa akihangaika huku na kule
kutafuta ajira hivyo niliamua kumsaidia ili aweze kufanikiwa kupata
kazi. Baada ya kumueleza Joyce alifurahi sana na haraka alikwenda
kupeleka vyeti vyake na baadaye alifanyiwa usaili, na baada ya wiki
mbili tu alifanikiwa kupata kazi katika kampuni ya Sigara. Maisha
yaliendelea na sasa wote tulikuwa na kazi. Siku moja nikiwa nyumbani
nimepumzika Joyce alifika huku akionekana kuwa mwenye furaha sana "Mary
rafiki yangu, sasa mambo yangu ni mazuri, yaani hapa nilipo ninafuraha
sana, yaani hata sijui nianzie wapi kukueleza".
Nilimtizama huku
nikionyesha tabasamu zito nikiwa na shauku kubwa la kutaka kujua kwanini
Joyce alikuwa amefurahi kiasi kile "Ehee niambie rafiki kuna nini tena"
Aliguna kidogo kisha akasogea na kuketi karibu yangu huku akinionyesha
karatasi ambayo ilikuwa na maandishi ambayo nilishindwa kuyasoma kwa
haraka kwasababu Joyce alikuwa akihangaisha mikono yake bila kutulia,
"Yaani Mary mwenzio naenda Marekani umeona hii barua ni kwamba kuna
nafasi za kazi, zimetoka hivyo na mimi nimejaza fomu na hivyo
nimechaguliwa kwaajili ya kwenda kusoma na kufanya kazi, hapa nilipo
ninafuraha isiyo na kifani".
Nilifurahi sana kusikia rafiki yangu
kipenzi ndoto zake zinakamilika "Hongera sana (my dear)mpendwa, Mungu
akutangulie, katika kila jambo hiyo ni hatua kubwa sana, sasa mbona
hukuniambia na mimi mapema ningejaribu bahati yangu?" Joyce alicheka na
kusema "Unajua hizi nafasi zilikuwa chache na maalumu kwa wafanyakazi
wa kampuni ninayofanyia kazi hivyo hata ningekuambia usingeweza
kufanikiwa" Tulizungumza sana siku hiyo na nilimtakia kila la heri
baadaye aliondoka.
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu
aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na
kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke
wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa
tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake
yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna
ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi
nimwam
bie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa
utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu
badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa
nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya
akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si
mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi
kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu
kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye
ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa
jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali
kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary.
Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote
yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke
wangu!
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya alhamisi
nilipokutana naye kwa mara ya kwanza.Siku hiyo nilikuwa shuleni,alipokuja
shuleni kwetu.
Nilikuwa nje nikimalizia muda wa mapumziko,niliegemea kwenye
nguzo ya nje ya darasa letu,nimeinama nikiwaza juu ya ombi la John la kuwa naye
kimahusiano ya kimapenzi aliloniambia jana.
Nilipoinua
kichwa changu nilimwona mvulana mgeni katika macho yangu, mrefu na mwenye mwili
mwembamba,alikuwa amependeza sana.Si kwamba alivaa vipi ,ni jinsi ya rangi ya bluu
na fulana nyekundu,ndiyo iliyomfanya aonekane simati na kunitoa udenda.
Alipozidi kusogea karibu na kuonekana barabara mapigo ya moyo yalibadilika nikaona yanaanza
kwenda mbio mbio.Mfumo wangu wa damu ulibadilika,damu ikaanza kwenda kwa kasi
zaidi.
Ni upendo mkubwa uliojitokeza baada ya kuonana na Krisi,moyo
wangu ulivutiwa sana na mwonekano wake tu,ingawa sikuwa namfahamu tabia yake na
hata jina ,sikulifahamu ,lakini hayo yote hayakuwa na nafasi katika fikra
zangu.
LABDA haitakuwa sahihi nikilalamika sana maana sina wa kumlaumu.
Haitakuwa na maana nikilia sana huenda chozi langu linazidi kumkera mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi.
Natamani sana kumwomba mungu msamaha lakini si sawa kama sitatubu katika dunia kwanza!!
Ewe mwenye moyo nisikilize kwa makini, nakuandikia haya katika sikukuu
ya Iddi maana nayakumbuka machungu mengi sana, si machungu ya kuletewa
na mtu bali kwa uzembe wangu mwenyewe. Uzem,be wa kuchanganua mambo na
kujua zipi pumba na upi mchele.
Nipe sikio na moyo wako sasa, maana
mimi ni mfano kwenu. Mfano mbaya usiofaa kuigwa bali kuwafunzi watoto
wenu na vizazi vijavyo. Yawezekana pia mimi ni mfano kwako wewe ili kama
hujaingia shimoni usiingie kamwe!!!
MNAMO miaka mitatu
iliyopita, nikiwa nimemaliza shahada yangu ya kwanza ya ualimu.
Nilibahatika kukutana na msichana ambaye sijui nimwelezee vipi ili
utambue kuwa alinivutia.
Tabia zake tangu aliponipisha kiti niketi
ndani ya daladala baada tu ya kutambua kuwa mimi ni mrefu sana hivyo
naumia sana kuinama katika daladala ile.
Msichana wa mjini kumpisha kiti kijana mwenzake ndani ya daladala? Ilinistaajabisha.
Ningekosa ustaarabu iwapo nisingetoa shukrani kwa mwanadada yule, na
hapo ukaribu wetu ukaanzia. Akanipa namba yake ya simu bila kusita.
Akanieleza kuwa anakaa Gongo La mboto nami nikamweleza kuwa ni mwenyeji
wa Dar lakini nipo Mombasa kikazi na nd’o kwanza nimepata ajira.
Bahati nzuri aliwahi kufika Mombasa pia, hilo jambo likatuweka karibu zaidi.
Hata nilipofika nyumbani na kuwasimulia watu wakanieleza kuwa huenda ni
bahati yangu na huyo ni mke ameletwa katika namna ya maajabu.
Hapo zamani za kale katika nchi moja Afrika, paliishi mama mmoja
ambaye alikuwa mjane. Muda mfupi tu kabla ya mumewe kufariki walijaliwa
mtoto mmoja wa kiume ambaye huyo mama alimlea kwa shida na taabu nyingi.
Hata hivyo mama na mtoto wake walipendana ipasavyo. Hapo katika kijiji
chao kulikuwa pia na tajiri mmoja ambaye alikuwa bahili na katili kweli.
Yule kijana maskini alikwenda kwa tajiri kuomba kazi. Tajiri alimwambia
kwamba alikuwa na kazi kwake na angemlipa vizuri sana.
Kijana alifurahi kusikia hivyo na akamwuliza tajiri kwa furaha.
"Kazi gani hiyo utanipa mheshimiwa? Mimi nitaifanya vizuri mpaka hata wewe utafurahia."
Tajiri akamwambia, "Ukilala katika maji baridi sana usiku mzima,
nitakupa shillingi laki moja." Ulikuwa wakati wa baridi sana kwamba maji
ya ziwa karibu yagandamane kuwa theluji kwa baridi.
Lo! Kijana hakufikiria angeweza kuwa na pesa nyingi hivyo katika
maisha yake. Tamaa ya kutaka kumsaidia mama yake ambaye wakati huo
alikuwa mgonjwa na mzee, ilikuwa kubwa sana kwa hivyo akakubali bila
kufikiria. Mama aliposikia habari hizo karibu azimie kwa wasiwasi na
huzuni.
"Mwanangu sitaki uhatarishe maisha yako kwa sababu ya pesa. Mungu
yuko nasi na hajatuacha hata siku moja tukalala njaa. Atazidi kufanya
hivyo hivyo. Je, ukifa nitabaki na nani mwanangu? Mimi mzee sasa wala
sijiwezi!" Kijana alimjibu,
"Mama usiwe na wasiwasi wala woga wo wote! Nitaweza kabisa kulala
kwenye maji baridi mpaka asubuhi na siwezi kufa" Mama bado alizidi
kubisha, lakini kijana alisisitiza kabisa kwamba lazima afanye hiyo kazi
ambayo itawaondolea shida zote za kifedha, kama alivyoona yeye.
Mama mmoja baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kushika mimba, aliamua
kwenda kwa mchungaji mmoja ambaye alitoka nchi ya mbali na kuja pale
mtaani kwao akiwafanyia watu miujiza mbalimbali kupitia maombi yake na
mama akaomba kuombewa ili apate mtoto.
Mchungaji yule alimfanyia ibada fupi na miezi michache baadae yule mama
alibahatika kupata mimba na kuibeba kwa miezi tisa kisha akajifungua
salama mtoto wa kiume.
Mama yule aliendelea kumtunza mwanae kwa kumnyonyesha ingawa kila
alipomnyonyesha mtoto yule mama aliishiwa nguvu na kulala kwa muda kabla
ya kuamka na kuendelea na kazi.
Jambo lile lilimshtua sana mama lakini akafikiri labda ni tatizo la kawaida kwani hakuwahi kuwa na mtoto.
Akaamua amwanzishie kumpa maziwa na kumwomba msichana wake wa kazi kuwa
awe anampa maziwa pindi yeye yupo kazini na akawa akinunua maziwa lita
tatu ili yaweze kukaa kwa siku tatu.
Maajabu ni kwamba lita tatu ziliisha kwa siku na mama kwa kuwa alipenda
kwenda na bajeti hivyo alimkaripia msichana wa kazi na kumpiga sana kwa
kumaliza maziwa lita tatu kwa siku.
Binti alilalamika sana na kusema mama huwa nayachemsha na kuyaacha
mengine kwenye sufuria kisha kidogo namnywesha mtoto na ninaendelea na
kazi kabla ya kuja kuangalia na kuona mazima yameisha kwenye sufuria.
Mama hakuamini na binti akaamua kuweka mtego ili aone kama ni majirani wanamfanyia visa au kuna kitu ambacho hunywa maziwa yale.
SHAMRA shamra zilizidi kurindima kwa fujo katika ukumbi wa Sabasaba
wilayani Temeke, hakika maharusi walikuwa wamependeza na utakuwa mchoyo
wa kuzaliwa usingewapongeza waliotumia ubunifu wa hali ya juu kuupamba
ukumbi ule nao ukapambika.
Kila mmoja alitabasamu bila kujalisha linatoka moyoni ama ni la kuzugia!!
Wanawake walipiga vigelegele na wanaume walipiga mbinja kila muda ambapo msema chochote aliamuru!!
Naam!! Ilikuwa sherehe ya aina yake ya kuwaunganisha Maria na Christian kuwa mwili mmoja!!!
Chris alikuwa mwenye furaha sana alipopewa nafasai ya kusema chochote,
alizishukuru pande mbili akianza na ule upande wa ukweni akawashukuru
kwa zawadi ya mke mwema…..kisha akageukia upande wa pili na kuwashukuru
wazazi wake waliomkuza na kumpa elimu dunia pamoja na ile ya darasani!!!
Hatimaye msema chochote akamkabidhi kipaza sauti Maria!!
Ukumbi mzima ulitambua kuwa Maria hakuwa akitabasamu kutoka moyoni lakini bado hakuna aliyejua kwanini alikuwa katika hali ile.
Maria akashika kipaza sauti mbele ya umati na kuanza kuzungumza.
“Imekuwa safari ndefu sana hadi kuifikia siku hii ya leo…nikimtoa
mwenyezi Mungu katika safari hii ninaye mtu mwingine muhimu katika dunia
hii wa kumshukuru!! Ni mtu mmoja tu nasisitiza pasipokuwa na unafiki
wowote!!
Namshukuru mama yangu…mama yangu wa Kambo” akasita kidogo ukumbi nao ukawa kimya!! Kimya kikuu…Maria akaendelea.
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula,
nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu
alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena
nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya
kuanza kufumbua kinywa changu.
Lakini ilibidi nimwambie ili ajue
nilikuwa nikifikiri nini juu yake.Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema
kwa utulivu . Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake
aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini ?’ Sikumjibu swali lake.
Kutojibu kulimfanya akasirike . Akatupa kijiko na akanikaripia , ‘wewe
si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia
kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye
ndoa yetu . Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya
kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa
Husna. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Husna. Kwa
kweli nilimdharau mke wangu !Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya
kosa , niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu)
angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu.
Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.Mke ambaye tumeishi
nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu .
UNAJUA jina la mwanamume mwenye nguvu
kuliko wote? Ni mwamuzi Samsoni. Yehova anampa Samsoni nguvu hizo. Hata
kabla ya Samsoni kuzaliwa, Yehova anamwambia mama yake hivi: ‘Upesi
utazaa mwana. Ataongoza kuokoa Israeli kutokana na Wafilisti.’
Wafilisti ni watu wabaya wanaoishi Kanaani. Wana wanajeshi wengi, na
wanawaumiza Waisraeli sana. Wakati mmoja, Samsoni anapokwenda kwa
Wafilisti, simba mkubwa anatokea akinguruma kukutana naye. Lakini
Samsoni anamwua simba huyo kwa mikono yake tu. Pia anaua mamia ya
Wafilisti wabaya.
Baadaye Samsoni anapendana na mwanamke,
Delila. Viongozi Wafilisti wanaahidi kwamba kila mmoja wao atampa Delila
vipande 1,100 vya fedha akiwaambia kinachompa Samsoni nguvu nyingi
hivyo. Delila anataka fedha zote hizo. Yeye si rafiki wa kweli wa
Samsoni, wala wa watu wa Mungu. Anazidi kumwuliza Samsoni kinachompa
nguvu nyingi hivyo.
Mwishowe, Delila amshawishi Samsoni. Naye Samsoni anamwambia siri ya
nguvu zake, akisema: ‘Mimi sijanyolewa nywele. Tangu kuzaliwa kwangu,
Mungu alinichagua niwe mtumishi wake wa pekee, yaani, Mnadhiri.
Nikinyolewa nywele, nitapoteza nguvu.’
nikiwa nimekaa leacture room
nikimuangalia msichana aliyekaribu
yangu,niliyekuwa nikimuita
"Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia
nywele zake nzuri na sura yake ya
upole huku nikitamani awe
wangu,lakini yeye hakuwa
akitamani hilo na nilikuwa
nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu
na kuniomba notes za siku ya
nyuma kwa sababu hakuweza
kuingia darasani hiyo siku
Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo
haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo
zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio
ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye
sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya
Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu.
Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake
kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa
kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile,
akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa
ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma.
Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia
kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa
‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia
vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika
mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka
kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya.
Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na
mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu
mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda
kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya
mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao
wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo
mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale.
Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha
kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla
nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo
lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule,
nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa
umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea
kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa
aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi
tulipomaliza bado alisimamia msimamo.
"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba
maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru
alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi.
Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya
nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha
sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu
mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa
msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi
huyo niliyeamini kuwa ni mume
wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini
aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini
alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa
mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye
atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilikuwa
katika wakati mgumu sana, kwani hakuna aliyekuwa akinijali, lakini
sikukata tamaa kwakuwa niliamini Mungu yupo pamoja nami. Kuna wakati
nilijikuta nakata tamaa kutokana na watu wengi kunizungumzia maneno
yasiyokuwa na ukweli wowote. Maisha yangu yalikuwa yamezungukwa na
marafiki wengi ambao kwa kiasi kikubwa nilikuwa nikiwaonyesha upendo na
kuwaamini kuwa ni watu wa muhimu sana katika maisha yangu, Lakini kumbe
haikuwa vile ninavyofikiria walikuwa wamejivika ngozi ya kondoo lakini
mioyo yao ikiwa imejaa chuki juu yangu.
Katika Maeneo ya Vijana Kinondoni
jijini Dar es salaam nilikuwa nikishi na Mama yangu mkubwa, kwani
sikubahatika kuishi na wazazi wangu Baba na Mama yangu walifariki nikiwa
mdogo sana. Mama yangu mkubwa alinilea vizuri sana hadi nilipomaliza
elimu yangu ya sekondari, na kufanikiwa kuanza chuo cha uhasibu. Nikiwa
chuoni nilikutana na marafiki mbalimbali.
Saida alikuwa ni rafiki yangu kipenzi
pale chuoni. Siku moja nikiwa najisomea Saida alikuja na kusema "Rozi
rafiki yangu, kuna jambo nataka kukuambia, lakini mwenzangu usije
ukamwambia mtu yeyote kuwa mimi ndiye niliyekueleza jambo hili"
Ilinibidi nishangae na kusema "Ni jambo gani hilo? Mbona unaniweka roho
juu. "Maneno yameenea hapa chuoni, watu wanakusema sana vibaya, yaani
sijui nianzie wapi kukueleza." Moyo wangu ulishtuka nikawa nimebaki
nashangaa "He! Watu wananisema vibaya? Kwani mimi nimefanya nini? Mbona
unanishangaza Saida embu kuwa muwazi uniambie ni kitu gani kinaendelea".
Saida aliguna kidogo nakusema "Rafiki
yangu, hivi ni kweli una uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wa hesabu.
Mr Ngowi, ndiyo maana unafaulu vizuri somo lake?" Ilinibidi niweke
daftari langu pembeni na kusema "Eti nini Saida, kina nani wanasema
hivyo, jamani mbona watu wanapenda kuzungumza maneno ya uongo, mimi sina
uhusiano wowote na mwalimu Ngowi" Saida akacheka nakusema "Basi watu
wengi hapa chuo wanajua ni kweli na anayesambaza hayo maneno ni Lina,
ila chonde chonde usije kunitaja" Nilijisikia vibaya sana siku hiyo
kwani ukweli ni kwamba sikuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwalimu.
Siku zilivyozidi kwenda maneno
yaliendelea na Saida alikuwa akija na kunieleza maneno ambayo
yanzungumzwa kuhusu mimi. Nilivumia hali hiyo bila yakumuuliza mtu
yeyote kwani nilikuwa sipendi ugomvi.Siku ya jumamosi na jumapili mara
nyingi nilikuwa nikienda kushinda nyumbani. Ilikuwa ni jumamosi moja
ambapo nilienda nyumbani na kumkuta mama yangu mkubwa akiwa amekasirika
sana. Nilimsalimia lakini hakuniitikia jambo ambalo niliona siyo la
kawaida.
Nilijaribu kumsalimia tena ndipo
aliponyanyuka na kunipiga kibao katika paji la uso wangu " Wewe
mwendawazimu, mimi nakulipia ada, halafu unaenda kufanya mambo ya ajabu
chuoni, hivi wewe ni mtu wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwalimu
wako? Tena nimesikia huwa haulali chuoni kila siku unakuja kuchukuliwa
na wanaume tofauti, yaani unabadilisha wanaume kama nguo. Hivi hii tabia
ya ukahaba umeipata wapi?" Nilibaki nimeduwaa huku nikmisema "Hapana
Mama mimi sina tabia hiyo, siwezi kufanya hivyo, unanionea Mama" Nililia
kwa uchungu kwani Mama aliendelea kunigombeza huku akinipiga makofi ya
usoni bila ya kunisikiliza.
Maisha yangu yalikosa furaha kwani kila
kukicha yalikuwa yakiibuka mambo tofauti, lakini sikujua nani ambaye
anaweza kunifanyia yote haya. Kwani moyoni mwangu nilikuwa najua
sikuwahi kumkosea mtu yeyote.
Baada ya wiki mbili huku nikiwa sina
maelewano mazuri na familia yangu.Siku hiyo nilikuwa chumbani
nimepumzika pale chuoni alikuja Lina huku akiwa na kikosi cha marafiki
zake. "Tumechoshwa na maneno yako, Rozi wewe mwanamke ni mnafki sana,
kwanini unapenda kutufuatilia maisha yetu, unanisema vibaya kwa watu
kuwa mimi na uhusiano wa kimapenzi na walimu, eti ndiyo maana nafaulu
vizuri, ukaona haitoshi ukaenda kumwambia mpenzi wangu mimi namsaliti.
Kwanini unanifuatilia au unamtaka mpenzi wangu?". Aliongea Lina kwa
sauti ya jazba.
Nilinyanyuka pale kitandani na kuuliza
"Mbona siwaelewi, Eti unasema mimi nakusema vibaya, hivii unajua
unanishangaza wewe Lina yaani wewe unavyonizungumzia mimi vibaya,
unampelekea maneno ya uongo hadi Mama yangu mkubwa, umeona haitoshi
unataka kunisingizia mimi nakusema vibaya." Baada ya mimi kusema hivyo
wote walinyamaza kimya kwa muda huku wakitazamana, mmoja wao akauliza
"Nani amekuambia hayo maneno, acha uongo Lina hajawahi kukusema vibaya"
Kutokana na hasira nilizokuwa nazo kwa
wakati huo niliamua kumtaja Saida, ndipo wote wakabaki wakishangaa kumbe
Saida huyohuoyo ndiye aliyekuwa anawapelekea maneno kwamba mimi
namzungumzia vibaya Lina. Kwa wakati huo Saida alikuwa hayupo
tulimsubiri hadi aliporudi na sasa kila mmoja alimvamia kwa maneno
makali huku wakimwimbia kwa tabia yake mbaya ya kusema uongo na
kuchonganisha watu. Nilijisikia vibaya sana kwani mtu niliyemuamini kama
rafiki yangu ndiyo alikuwa na nia ya kunichonganisha na marafiki hadi
familia yangu. Aliniomba msamaha, mwanzoni ilikuwa ni vigumu kumsamehe
lakini baadaye niliamua kumsamehe na maisha yanaendelea SIJAPOTEZA
FURAHA YANGU.
Kuwa makini, usiamini maneno yote
unayoambiwa, na mtu yeyote yule ni vyema kuchunguza ili kuwa na uhakika
wa kile ulichoambiwa vinginevyo unaweza kugombana na watu kwa jambo
lisilokuwa na ukweli. wahenga wanasema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.
"Mbona
umepauka sana, au haujapaka mafuta, mmmh halafu unanenepa sana siku
hizi" Nilimtizama Ashura na kusema "Mbona mimi najiona nipo kawaida na
pia nimepaka mafuta." Huku akicheka kwa dharau Ashura aliingia ndani na
kuniacha nikiwa nimesimama kibarazani. Nilijiuliza maswali mengi kwanini
Ashura ananicheka nilijitizama huku nikihisi labda nina kasoro yoyote
katika mwili wangu lakini sikuiona. Basi nilimpuuza na kuendelea na
safari yangu.
Mimi ni mzaliwa wa Morogoro katika
familia ya watoto watatu, Baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata
nafasi ya kuendelea na elimu ya chuo kikuu Dar es salaam, Kutokana na
hali halisi ya maisha ya nyumbani nilipotokea wazazi wangu walikuwa
hawana uwezo, hivyo ilinibidi nimuombe rafiki yangu Ashura anisaidie
hifadhi katika chumba alichokuwa amepanga karibu na maeneo ya chuo.
Ashura alinikubalia na hivyo nilipata sehemu ya kuishi bila ya kutumia
gharama yoyote.
Kuna vijana walikuwa wamekaa kijiweni
huku wakizungumza, ghafla akapita kijana mmoja anaitwa Sudi na
aliwasalimia, huku akiwa anaendelea na safari yake kwa bahati mbaya
aliteleza na kuanguka, lakini hakuna hata kijana mmoja aliyenyanyuka na
kumsaidia wote waliangua vicheko na mmoja wao akisema "Huyu jamaa
atakufa kwa mawazo, si anaishi hapo mtaa wa pili kwa ndugu zake yaani
hawana chochote ni masikini sana kazi yao ni kuombaomba" Huku
wakiendelea kumcheka.
Sudi alinyanyuka na kuendelea na safari
bila ya kuzungumza chochote huku machozi yakionekana kumlengalenga
aliwaza moyoni mwake "Watu wengi wananidharau kutokana na hali duni ya
maisha niliyonayo, eeh Mungu nisaidie" Pale kijiweni waliendelea
kuzungumza "Unajua umasikini ni mbaya sana, kwani siku zote ukiwa
masikini, basi ujue utapata shida sana, na ukizingatia yule aliyenacho
ndiyo anazidi kuwa nacho."
Mara nyingi nilikuwa nikimshauri sana Sara, kuachana na mpenzi wake
kutokana na mpenzi wake huyo kuwa na tabia mbaya. Ambapo wakati mwingine
alikuwa akimpiga sana. Siku hiyo nilikuwa nyumbani nimepumzika ghafla
nilisikia mlangoni kuna mtu anabisaha hodi kwa nguvu. "Suzi, Suzi,
naomba ufungue mlango John ananiuwa" Ilikuwa ni sauti ya Sara
nilinyanyuka haraka na kufungua mlango Sara alionekana kuumia maeneo ya
usoni nilishtuka sana kumuona katika hali ile "Hee! Umepatwa na nini
Sara, mbona hivyo kulikoni?" Nilimuuuliza huku nikimkaribisha ndani.
Aliingia na kuketi lakini bado alikuwa analia kwa uchungu huku akisema
"Yaani mimi kweli John ni wakunifanyia hivi, wakati nimemfumania na
mwanamke mwingine? Halafu ananipiga" Nilisogea na kuketi karibu huku
niki mliwaza "Pole sana Sara, lakini kwanini anakupiga, kwa kosa lipi
ulilomfanyia, huyu mwanaume ana kichaa heee! na wewe rafiki yangu
mwanaume kama huyo hakufai ni bora uachane naye kabisa. Embu tizama
umemfumania halafu anakupiga, usiwe mjinga kiasi hicho Sara wanaume
wapo wengi, kama yeye anakuona wa nini, basi ajue kuna wengine
wanafikiria watakupata lini. Mwanaume gani mshamba huyo usipoangalia ipo
siku atakuvunja mguu".
Jerome alikuwa na ndoto ya kuwa
mfanyabiashara mkubwa sana, Alikuwa ni kijana mchapa kazi na wakati wote
alikuwa makini sana. Katika maisha yake alisema kamwe hawezi
kuchanganya kazi na mapenzi. Kijana huyu alikuwa ni mkarimu mtanashati
na mwenye mvuto wa hali ya juu, baadhi ya wanawake walikuwa wakitamani
kuwa karibu naye lakini Jerome alikuwa na msimamo hakutaka kabisa
kujiingiza katika suala zima la mapenzi.
Akiwa anaendelea kazi zake ambapo kazi
zote alikuwa akizifanya akiwa anaishi Mkoa wa Dodoma. Baadaye alianza
kusafiri na kwenda katika mikoa mbalimbali hususani Mkoa wa Dar es
salaam ambapo alikuwa akikutana na wafanyabiashara mbalimbali.
Siku moja akiwa jijini Dar es salaam katika shughuli zake alikutana na
dada mmoja ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo na walifahamiana, na
kisha kubadilishana namba za simu.
Nimechoka
na kero za kila siku, sitaki kabisa yaani ni bora tu niondoke nirudi
kwetu" Stara Alikuwa anazungumza kwa sauti iliyoonyesha kuwa na uchungu
sana kutokana na tabia za mume wake ambaye alikuwa anachelewa kurudi
nyumbani na akirudi anakuwa amelewa sana. Hali hii ilikuwa inamuumiza
sana Stara ambaye alikuwa anavumilia kwasababu alikuwa anampenda mume
wake.
Maisha ya Stara na mume wake kabla ya
kuingia kwenye ndoa yalikuwa ni maisha yaliyojaa furaha na upendo,
lakini baada ya kuingia kwenye ndoa mambo yalibadilika, Kutokana na hali
hiyo Stara alikuwa akiumia sana ilifikia kipindi akawa anashindwa
kuvumilia kutokana na tabia ya mume wake kumpiga, na kuna wakati
alikuwa akirudi amelewa usiku wa manane alikuwa akimlazimisha Stara
kuwa naye kimepenzi kwa nguvu hata kama Stara akisema anaumwa, yeye
alifanya nguvu yaani alikuwa akimbaka mke wake kutokana na kumtaka
kimapenzi kwa nguvu bila ya kumuandaa. Stara aliumia sana.
Katika
maisha unaambiwa mvumilivu hula mbivu, kwani siku zote hakuna safari ya
maisha isiyokukuwa na changamoto,Monalisa aliolewa na Jerome na
kufanikiwa kupata watoto wawili walikuwa wakiishi katika nyumba ya
kupanga na kutokana na hali ya maisha walikuwa wamepanga vyumba viwili,
Watoto walikuwa wakilala sebuleni.Wakiwa wanaendelea kuishi huku
wakihangaika kutafuta pesa ya kujikimu katika maisha, Siku moja wakiwa
nyumbani majira ya saa moja jioni walisikia mlango ukibishwa hodi.
Monalisa alinyanyuka na kufungua mlango
kumbe alikuwa amekuja wifi yake ambaye alikuwa ambeba begi lake kubwa
na mfuko wa Rambo, Alimkaribisha ndani na kumsaidia kubeba begi. Wifi
huyu alikuwa ametokea Kijijini Morogoro na alifika kwa kaka yake ili
aweze kutafutiwa shule, Basi alikaribishwa vizuri bila matatizo yoyote,
Kutokana na nyumba kuwa ndogo ilimbidi ajumuike kulala pamoja na watoto
pale sebuleni ambapo walikuwa wakitandika godoro na kulala pamoja.
Maisha yaliendelea, huku wifi akiwa anaishi pale nyumbani, siku zote
alikuwa akiamka asubuhi lakini asimsaidie Monalisa kufanya kazi yoyote.
Hivyo Monalisa alikuwa akimka mapema
nakuandaa kifungua kinywa na wakati mwingine ilimbidi apike chakula
asubuhi kwaajili ya kuwaachia watoto halafu ndiyo aondoke kwenda kwenye
biashara yake ya kuuza samaki.Maisha yaliendelea hivyo hivyo ndipo
sikumoja Monalisa aliamua kumueleza mume wake tabia za mdogo wake kukaa
bila ya kufanya kazi yoyote na ukizingatia alikuwa ni msichana mkubwa,
Jerome alijaribu kumwelekeza mdogo wake bila mafanikio kwani sasa ndiyo
alileta mtafaruku zaidi kati ya Monalisa na wifi yake, sasa Wifi alianza
kununa bila sababu na kumchukia sana wifi yake.
Hali ile ilikuwa inamuumiza sana
Monalisa ambaye alikuwa akihangaika siku zote ili nyumbani watoto waweze
kupata chakula, na Mume wake alikuwa ni fundi seremala, na hata
alipokuwa akipata pesa mara zote alikuwa akimpa mdogo wake kwahiyo
ilimbidi Monalisa, ajibane sana katika kutafuta pesa kwaajili ya
matumizi ya pale nyumbani. Baada ya miezi sita kupita wifi yake Monalisa
vituko ndiyo vilizidi sasa alianza kuleta wanaume pale nyumbani. Siku
zote alikuwa akisubiri watoto wakiwa wameenda shule, na Baba na Mama
wakiwa wameenda kazini, na kutumia muda huo kuingiza wanaume, na huku
akitumia kitanda cha kaka yake bila ya kujali chochote, tabia hiyo
iliendelea hadi siku ambay
o Monalisa aligundua kuwa shuka lilikuwa
limechafuka na kumuuliza wifi yake ambaye alikasirika sana.
Huku akiwasingizia watoto walikuwa
wakicheza kitandani, lakini watoto walikanusha huku wakilia kuwa
wamesingiziwa. Baadaye Monalisa alipuuzia lakini wifi yake hakuacha hiyo
tabia, ndipo siku moja jirani aliamua kumueleza Monalisa kile
kinachoendelea akiwa hayupo.Monalisa alisikitika sana na sasa aliwaza
namna ya kumfumania wifi yake.
Siku hiyo alikwenda kazini kama kawaida
lakini hakukaa muda mrefu akawa anawasiliana na yule jirani ambaye
alimwambia kuwa muda huo kuna mwanaume amefika pale nyumbani. Moja kwa
moja Monalisa aliondoka kijiweni na kurudi nyumbani ambapo alimkuta wifi
yake akiwa amejipumzisha kitandani kwake na mwanaume huku wakifanya
starehe zao, Alishtuka sana na kuanza kumfokea huku akimtaka
aondoke."Wifi nimekuchoka, naomba uondoke, aibu gani hii jamani,
unawafundisha nini watoto wangu naomba uondoke sitaki kukuona kabisa"
Wifi kwa hofu alianza kulia na kuomba
msamaha kwa Monalisa asimueleze kaka yake.Lakini Monalisa alimuambia
haiwezekani amekwisha mvumilia vya kutosha lazima aondoke, Baadaye
Jerome aliporudi kutoka kazini Monalisa alimweleza kila kitu ndipo kaka
mtu alipoamua kumrudisha mdogo wake kijijini kwa kuchoshwa na tabia za
mdogo wake.Wifi aliomba msamaha, na Monalisa alimsamehe lakini
alimwambia ni vyema angerudi nyumbani Morogoro.
Alipomaliza
chuo tu Justa aliolewa na Mfaume kijana huyu alikuwa ni
mfanyabiashara, ambaye alikuwa akimpenda sana Justa. Mfaume alikuwa
akiishi na mdogo wake wa kike aliyekuwa anaitwa Leti kwa kipindi hicho
Leti alikuwa bado anasoma chuo. Baada ya Justa kuolewa sasa alihamia na
kuishi pamoja na mume na wifi yake, maisha yalikuwa mazuri kwani Mfaume
alikuwa anampenda sana mke wake. Kwa kipindi hicho Justa alikuwa bado
hajafanikiwa kupata kazi hivyo alikuwa ni Mama wa nyumbani huku akiwa
anaendelea kutafuta kazi.
Siku zote Mfaume alikuwa akiacha pesa za
matumizi pale nyumbani na alikuwa akimpa mdogo wake pesa hizo yaani
hata pale mke wake alipokuwa na shida ilimbidi amweleze wifi yake kwani
mume wake alikuwa akimpatia pesa zote za matumizi ya pale nyumbani mdogo
wake.Hali ile ilikuwa inamuumza sana Justa na ndipo alipoamua kumwambia
mume wake kuwa hapendezewi na tabia yake lakini mwanaume huyo hakutaka
kumsikiliza.
"Asante sana shemeji Beni kwa msaada
ulionipa, lakini nilikuwa naomba uniongezee kiasi cha shilingi laki tano
tu, kuna jambo nataka kulifanya, nimepungukiwa kidogo, naimani
utanisaidia". Alikuwa ni shemeji yangu ambaye ni kwa kipindi kirefu
nimekuwa nikimsaidia kuendeleza biashara zake, kwa wakati huo nilikuwa
sina kiasi hicho cha fedha "Ningependa kukusaidia shemeji lakini hali
yangu kiuchumi kwa sasa imeyumba ila usiwe na shaka nitafanya mikakati
ndani ya siku mbili tatu nitakupa hiyo pesa.lakini shemeji kuwa makini
sana na utumiaji wa pesa kwani kwa sasa pesa imekuwa ngumu kupatikana
hivyo ni vyema ukawa makini sana katika biashara yako". Baada ya
kumaliza mazungumzo shemeji alinielewa na kuondoka.
Kesho yake asubuhi ilikuwa ni siku ya
jumamosi ambapo siku hiyo si kwenda kazini, alikuja dada yangu akiwa
pamoja na mtoto wake mdogo wa kike. "Habari za masiku dada, karibu
sana" Dada alinitizama huku akisema "Kaka habari yangu si njema kwani
hapa nilipo, nimekuja kwako nina shida mtoto amerudishwa nyumbani
kwasababu ya anadaiwa ada, sasa kaka naomba unisaidie shilingi laki tatu
niweze kumrudisha mjomba wako shule, yaani hapa nilipo sina mtu
mwingine wa kumtegemea zaidi yako".
Nilikuwa nimeketi pale sebuleni huku
nikiwaza na nafsi yangu "Mhhh hapa nilipo leo nimeamka nina shilingi
elfu kumi na tano tu mfukoni mwangu sasa nitawezaje kumsaidia dada
yangu" Nilimtizama dada na kusema "Daah, hali ni mbaya sana dada yangu,
umenikuta sina pesa kabisa lakini embu subiri naweza kumkopa rafiki
yangu kiasi hicho cha pesa ili mtoto aende shule." Nilimpigia simu
rafiki yangu anaitwa Zuberi na kumuomba anikopeshe pesa kidogo, kwa
bahati nzuri nilifanikiwa hivyo nilimpa kiasi kile cha fedha dada.
Baada ya dada yangu kuondoka mke wangu
alikuja akiwa ametoka sokoni "Mume wangu imekuwa ni vizuri nimekukuta
kwani mama amenipigia simu alikuwa anataka kuongea na wewe" Basi moja
kwa moja mke wangu akampigia simu Mama mkwe wangu kisha akanipa simu
niongee naye. "Shikamoo Mama habari za hapo nyumbani" Mama aliitika kwa
sauti ya unyonge "Habari si njema mwanangu mwili unaniuma sana, halafu
sina pesa kabisa, naomba unitumie hela ya kununua mchele na sukari
pamoja na ya kwenda Hospitali" Nilikuwa nikimsikiliza kwa umakini na
baadaye nilimuahidi kuwa nitamtumia pesa kwaajili ya matibabu na
chakula. Nilikuwa sina hela ilinibidi nikope pesa kwaajili ya kumtumia
mama mkwe.
Baada ya siku tatu kupita yule shemeji
yangu alinipigia simu na kunikumbusha kile kiasi cha pesa alichoniomba,
kwa bahati nzuri siku hiyo nilikuwa nimefanikiwa kupata pesa katika
biashara zangu hivyo sikusita kumsaidia. Maisha yangu yalikuwa
yamezungukwa ndugu wengi waliokuwa wakinitegemea katika mahitaji
mbalimbali ijapokuwa nilikuwa sina uwezo mkubwa sana kifedha. Lakini
nilijitahidi kwa kila hali kuhakikisha nawasaidia.
Baada ya miaka mitatu siku moja nikiwa
natoka kazini nilipata ajali nikiwa naendesha gari aina ya Corola, na
kunisababishia kuvunjika miguu, nilikuwa katika wakati mgumu sana kwani
nilikuwa sina uwezo wa kufanya kazi tena.
Na sasa nilikuwa nahitaji msaada kwa
ndugu zangu, lakini chakushangaza wale ndugu niliokuwa nawasaidia hata
sikumoja hakuna aliyekuja kunisaidia kwa chochote, walikuja kunisalimia
maramoja tu na baada ya hapo sikumuona tena ndugu yeyote. Siku moja
alikuja shemeji yangu na Mama mkwe kwa nia ya kumshauri mke wangu
aniache kwani sina uwezo wa kumsaidia. Niliumia sana moyoni "Inamaana
leo hii mimi Beni, naonekana sifai baada ya kupata ajali, na mbona
nilikuwa nikiwasaidia sana, hivi ni kweli wananichukia kiasi hiki. Mungu
nisaidie nipone, ama kweli binadamu hawatabiriki."
Mke wangu, alikuwa na msimamo na hivyo
hakuniacha aliendelea kuwa na mimi hivyohivyo. Ndugu zake walimtenga
kabisa, kwasababu yangu.Maisha yalliendelea baada ya mwaka mmoja
kupita, hatimaye nilipona kabisa nakurudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilirudi katika kazi yangu ya awali bila matatizo. Kwani nilipokelewa
vizuri na sasa nilipandishwa cheo. Maisha yangu yalirudi katika ramani
nzuri, wale ndugu walionikimbia wakati naumwa, baada ya kusikia kuwa
nimerudi kazini. haikuchukua muda walianza kuja kunitembelea tena
wakijidai wamekuja kunijulia hali.Lakini kwasababu tayari nilikuwa
nimejifunza mambo mengi hivyo nilijua namna gani naweza kuishi nao.
Safari hii nilikuwa makini zaidi. Sikutaka kulipiza kisasi naishi nao
vizuri.
AMA KWELI BINADAMU HAWATABIRIKI, ANAWEZA KUKUPENDA UKIWA NACHO UKIWA HAUNA KITU ANAKUKIMBIA.
Ritha alikuwa ni msichana mrembo sana,
kila aliyemtizama alivutiwa na urembo alionao, na hata yeye alijitambua
kuwa ni mrembo. Katika maisha yake Ritha alikuwa anapenda sana vitu
vizuri na vinavyokwenda na wakati kama nguo, viatu, simu na vitu vingine
kadha kwa kadha. Lakini wazazi wake walikuwa hawana uwezo wa kumnunulia
vitu vyote hivyo.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, kwa
bahati mbaya hakufanikiwa kuendelea na kidato cha sita na hivyo wazazi
wake waliamua kumtafutia chuo.Akiwa anasoma chuo alikutana na marafiki
wa aina mbalimbali na marafiki zake wakubwa walikuwa ni wale ambao
wametokea katika familia ambazo wanajiweza yaani matajiri. Kutokana na
wazazi wao kuwa na pesa walikuwa wakimiliki simu nzuri, na kompyuta
(laptop) lakini kwa upande wa Ritha alikuwa hana hata simu ya mkononi,
alitamani sana kuwa na maisha mazuri kama ya wenzake.
Siku moja akiwa anatoka chuo kuelekea
nyumbani alikutana kaka mmoja aliyekuwa anaendesha gari aina ya Alteza
"Mambo mrembo, unaelekea wapi mamii" Yule kaka alimwita Ritha huku
akipunguza mwendo wa gari lake. Ritha alimtizama yule kaka na kusema
"Hapana asante, nitapanda tu daladala" Yule kaka akaendelea kusema
"Samahani lakini mrembo,nakuomba mara moja kuna jambo nilikuwa nataka
nikuulize" Basi Ritha akasogea karibu "Uliza tu hakuna tatizo" Kumbe
yule kaka alimwita kwa ukaribu ili ambembeleze apande kwenye gari yake.
Haikupita muda Ritha alikubali kupanda kwenye lile gari na waliendelea
kuzungumza na kufahamiana.
Yule Kaka alikuwa ni mfanyabiashara,
anaitwa Godson.Kutokana na Ritha alikuwa hana simu ya mkononi Godson
alimuahidi kumnunulia simu, na kesho yake angempelekea pale chuoni.
Baada ya kumfikisha Ritha maeneo ya nyumbani, alimpatia kiasi cha
shilingi elfu hamsini "Kiasi hiki kidogo cha pesa kitakusaidia, kwa
nauli siku ya kesho, nimefurahi sana kukufamu Ritha, wewe ni mrembo
ukinipa nafasi katika moyo wako, nakuahidi utafurahi sana" Ritha huku
akiuma vidole vyake kwa aibu akapokea ile pesa na kusema "Asante sana
Godson, ila naomba ukanishushe kwa pale mbele hapa Mama akiniona itakuwa
balaa" Basi akasogea mbele kidogo na kumshusha.
Ritha alikuwa anatabasamu huku
akizungumza na nafsi yake "Jamani, leo ni siku yangu ya bahati, huyu
kaka anaonekana ni mtu mwenye pesa sana, yaani amenipa shilingi elfu
hamsini ijapokuwa sijamjibu chochote kuhusu ombi lake, mmmh yaani huko
chuoni watanikoma, kwanza hii pesa niifiche vizuri, nikienda Mwenge
nanunua viwalo kwa kwenda mbele" Siku hiyo Ritha alikuwa na furaha
sana. Kesho yake kama kawaida alikwenda chuoni, alipotoka tu alimkuta
Godson anamsubiri.
Moja kwa moja walisalimiana na
alimpakia katika gari lake wakiwa ndani ya gari Godson alimpa Ritha simu
nzuri ya mkononi aina ya samsung galaxy. Ritha kwa furaha alimkumbatia
Godson huku akimbusu na kusema "Asante sana, jamani nimefurahi sana,
kweli nimeamini unanipenda Godson" Huku akicheka Godson akasema
"Nimekupenda sana Ritha, ukiwa na mimi kila kitu unachokitaka utakipata
nipo kwaajili yako".Na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mahusiano ya
kimapenzi kati ya Ritha na Godson.
Maisha ya Ritha yalibadilika, kwani
alianza kuvaa nguo za gharama na alikuwa hapandi daladala tena sasa
alikuwa akijakuchukuliwa na kupelekwa chuo kila siku. Na hata wazazi
wake walipokuwa wakimuuliza na kumkanya alikuwa awasikilizi aliwadharau
na kuona Godson pekee ndiyo wa muhimu katika maisha yake. Aliishi maisha
ya starehe sana na kuwadharau watu wengine bila ya kujali chochote.
Hata marafiki zake walikuwa wakimshangaa "Mmmh ama kweli watu
wanabadilika, sikuhizi Ritha anaringa sana tokea ampate huyo bwana
mfanyabiashara" Walikuwa wakizungumza marafiki zake.
Baada ya miezi sita Ritha alipata
ujauzito na kuamua kumwambia Godson ambaye alimwambia asijali atamlea
vizuri.Basi akawa na kiburi kuwa ataolewa na Godson.Baada ya siku mbili
tatu Ritha akiwa hana hili wala lile, mara alipita muuzaji wa magazeti
na moja kati ya yale magazeti ukurasa wa mbele kulikuwa na picha ya
Godson na habari ikisema "Mfanyabiashara jambazi asotwa rumande" Ritha
hakuamini alichokiona akasogea karibu na kununua lile gazeti kisha
kusoma kwa umakini. Ni kweli habari ile ilimuhusisha Godson kutokana na
kosa la ujambazi.
Akiwa anaendelea kusoma ile habari
akagundua kuwa Godson alikuwa na mke na watoto watatu. "Mungu wangu,
inamaana Godson ni jambazi, na tena kumbe alikuwa na mke? Mama yangu
nimekwisha.Nitafanya nini mimi na nina mimba ya miezi minne sasa na
nyumbani lazima nitafukuzwa najuta mimi TAMAA IMENIPONZA. Alikuwa
anaongea mwenyewe kama mtu aliyechanganyikiwa.
Baada ya mwezi mmoja kupita hali
ilizidi kuwa mbaya kwani mawasiliano na Godson hayakuwepo tena. Na sasa
aliwaomba msamaha wazazi wake na bila hiana wazazi walimsamehe.Hivyo
walimlea hadi alipojifungua salama mtoto wa kiume. Na maisha ya Godson
haikuelewweka yaliishia wapi kwani watu wengine walikuwa wanasema kuwa
baada ya kuachiwa huru alihamia nchi nyingine pamoja na familia yake.
Nilijaribu
kumuita lakini hakuniitikia na hata nilipomsogelea aliendelea kutembea
bila ya kusimama. Nilijisikia vibaya sana, kwani nilijiona nimedharaulika.
Hata watu waliokuwepo karibu walinitizama kwa nyuso za kuonyesha kuwa
wananionea huruma. Nilibaki nikizungumza na nafsi yangu. "Hivi ni kweli Lema
anaondoka na kuniacha, hapana siwezi kuamini nilimuamini kwa moyo
wangu wote".
Nilibaki
nalia huku nikijisemea na moyo wangu "Ama kweli dunia hadaa, ulimwengu
shujaa na asiyesikia la mkuu huvunjika mguu. Leo hii naumbuka kwa yote
haya yaliyotokea katika maisha yangu, lakini mbona sijui kosa langu,
inamaana ni kweli amenibadilikia kwa kiasi hiki. Lakini nakumbuka watu
wengi walinikanya kuhusu tabia ya Lema lakini mimi nilikuwa nafanya
mambo yangu kwa siri sana.
Tizama sasa nabaki
naumia na kuteseka peke yangu. Maisha yangu yote nilimuamini mwanaume
huyu. Ndugu, jamaa na marafiki walinikanya lakini nilihisi labda
wananione wivu leo hii najuta kwani siamini kama kweli Lema amenitendea
yote haya. Alikuwa amejiinamia chini Salima huku akilia kwa uchungu.
Maumivu makali moyoni mwangu eeh Mungu nisaidie.
Sikuamini
kilichotokea, lakini ndiyo hali halisi maji yamekwisha mwagika
hayazoleki tena.Nikiwa naendelea kuwaza alikuja rafiki yangu kipenzi
Anna na kunishika begani huku akisema "Pole sana Salima muombe sana
Mungu atakusaidia" Wakati Anna akiniliwaza machozi yaliendelea
kunibubujika kwa wingi katika paji la uso wangu. Baadaye nilinyanyuka na
kuelekea nyumbani taratibu.Maisha yangu yamekuwa na mtihani
mkubwa sana. Baada ya kukutana na Lema mwanaume ambaye nilifikiri
atakuwa ndiye chaguo la maisha yangu. Lakini haikuwa hivyo nikikumbuka
siku ya kwanza tulikutana nikiwa natoka kazini kuelekea nyumbani nikiwa
naendesha gari langu aina ya Rav 4.
Katika maeneo ya Posta jioni usafiri
huwa ni wa shida sana.Katika kituo cha daladala kulikuwa na watu wengi
wakisubiri usafiri huo.Mimi nikiwa katika foleni kaka mmoja alikuja
karibu na gari yangu na kunisemesha "Samahani dada, unaweza kunisaidia
lifti" Nilimtizama yule kaka na kusema "Mimi naelekea Kijitonyama, kwani
wewe unaenda wapi?" Akanijibu kwa haraka "Naelekea hukohuko dada yangu
naomba unisaidie" Haikuwa kawaida yangu kuwapa lifti watu barabarani
hususani mtu nisiyemfahamu lakini niliamua kumsaidia huyu kaka.
Siku
moja Lema aliniomba tutoke pamoja kwani kuna jambo angependa
kunieleza. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha kwangu kwani nilikuwa
napenda sana kuwa karibu na Lema wakati wote.Tukiwa tumeketi maeneo ya
Makumbusho, Lema hakusita kuniambia juu ya hisia zake "Nikikutizama
Salima wewe ni mwanamke mrembo sana, wakati mwingine
najiona kama sistahili kuwa karibu yako lakini siku zinavyozidi kwenda,
upole na ukarimu wako unanifanya nikupende zaidi.
Natamani ungekuwa
mpenzi wangu yaani uwe furaha ya milele katika maisha yangu, nakupenda
sana Salima." Huku akiwa ananitizama alisema Lema.Mimi nilikuwa
nimejiinamia kwa aibu "Asante Lema, hata wewe ni kijana mzuri sana.Ila
siamini kama hauna mwanamke unayempenda." Lema alitabasamu nakusema
"Nulijua utaniuliza hivyo, ni kweli nishawahi kuwa mpenzi lakini
tulitenganana ni muda mrefu sasa niko peke yangu. Lakini moyo wangu
umekutana na mwanamke mwenye kila sifa nilizokuwa nazihitaji ni wewe
Salima naomba unipe nafasi katika moyo wako" Moyoni mwangu nilikuwa
nikiwaza kwa kiasi gani nilikuwa natamani Lema awe mpenzi wangu na sasa
hatimaye ndoto zangu zimekamilika.
Tulizungumza na baadaye
nilimwambia Lema anipe muda nitafakari juu ya ombi lake. Baada ya wiki
moja hatimaye tulifungua ukurasa mpya wa mapenzi motomoto. Nilimpenda
sana Lema kwa moyo wangu wote. Nikiwa katika mahusiano ya kimapenzi na
Lema sikuwahi kuwaambia marafiki wala ndugu zangu. Mapenzi haya
niliyafanya siri kwa imani kwamba ipo siku Lema atakuja kujitambulisha
nyumbani. Baada ya miezi mitatu, siku moja nilikutana na rafiki yangu
mmoja anaitwa Sindy tulisalimiana "Jamani Salima nilikuwa nakutafuta
sana, vipi mbona simu yako nikikupigia sikupati hewani au umebadili
namba".
Ni kweli nilikuwa nimebadilisha namba ya simu akaendelea
kuzungumza "Unajua nilikuwa nakutafuta nikupe taarifa za msiba wa
Belinda, si unajua alikuwa anaumwa sana" Nilishangaa kwani Belinda
nilikuwa nikimfahamu "Maskini jamani, sikuwa na taarifa daah " Sindy
akasema "Ndiyo hivyo ndugu yangu, huyu Lema atawamaliza wadada wa mjini"
Nilihisi labda nilikuwa sijamsikia vizuri na kusema "Eti umesema Lema!
Atawamaliza wadada wa mjini?".
Niliuliza kwa shauku lakutaka kujua ni
Lema yupi "Inamaana wewe humjui Lema kijana mmoja mtanashati. Anaishi
karibu na maeneo ya pale kwenu yaani yule kijana anajijua kabisa ni
muathirika lakini huwa anawaambukiza wadada wa mjini kwa makusudi"
Nilihisi kuishiwa nguvu lakini ilinibidi nijikaze ili Sindy asielewe
chochote.
Baada ya Sindy kuondoka, nilijikuta machozi
yakinitoka na kuwaza sasa nitafanyaje kumbe Lema alikuwa na tabia chafu
zilizojificha. Akili ikanituma niende kupima afya yangu kwanza. Maskini
sintokaa nisahau ni kweli nilikuwa nimeathirika na moja kwa moja
nilimjua aliyeniambukiza virusi vya UKIMWI na sasa nilirudi nyumbani
huku nikiwa nimekata tamaa kabisa. Nilipofika nikiwa nmeketi kibarazani
huku natafakari ghafla alipita Lema akiwa ameongozana na mwanamke
nilimwita lakini hakuniitikia na hata niliposogea karibu alijifanya kuwa
hanijui kabisa. Moyoni mwangu nilibaki naumia na kujuta kumuamini Lema
kijana ambaye ni tapeli wa mapenzi na sasa ameniacha na maumivu ya
milele.
Usimuamini mtu kwa haraka fahamu kuwa Majuto ni Mjukuu. na pia kumbuka usiache mbachao kwa msala upitao.
Kijana
mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa
akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea
kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.Siku moja dada huyo
akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje
nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake
limekubaliwa.
Akiwa
nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana
na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana
alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea
kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku
akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika,
alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake.
Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu
aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba
maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo,
aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha
umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa
(mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema
"Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana." Yule
dada alitabasamu na kusema "Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito
wangu, samahani kwa usumbufu wangu".
Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza "Hakuna tatizo, usijali
kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina...." Kabla
hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku
akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula
kungu "Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri,
nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda"
Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema "Chochote tu, zawadi ni zawadi,
alimradi kuwe na mapenzi ya kweli" Dada yule alitabasamu na kusema "Ni
kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi, nitampenda maisha yangu
yote" Kaka yule akauliza "Utampenda? Nani huyo"
.
Yule dada alitabasamu tena na kusema "Samahani, rafiki nilikuwa
sijakuambia, wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu
ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi,
nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia" Yule kaka alibaki
amepigwa na butwaa, "Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo."
Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita
ili ampatie kadi bila ya mafanikio
Kulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa tajiri sana, Mzee huyu alibahatika kuwa na binti mmoja na ambaye alimpenda sana na hata kumwandika kuwa mrithi wa mali zake zote pindi mzee atakapoiaga dunia.
Mzee huyu alimiliki biashara kubwa sana sana na zenye kuingiza kipato kikubwa na aliogopeka sana sana katika eneo hilo hasa kwa kwa utajiri wake na ukatili wake pia.
Siku moja mzee huyo alipata taarifa kuwa mtoto wake wa pekee alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja ambaye anatoka katika familia isiyojiweza na tena ya kimaskini sana,na wazai wake walikuwa wakifanya kazi katika moja ya mashamba ya tajiri huyo.
Yule tajiri alijawa na hasira na kuona kama ilikuwa ni fedhea kubwa sana kwa familia yake na akamuita binti yake na alipomuuliza binti yake alikubalia, mzee kwa hasira akawafukuza wale wazee na kuahidi kutoa fedha nono kwa polisi yeyote atakaye mtia mbaroni kijana Yule.
Basi
kijana Yule ikabidi amfuate binti na kumwambia hali halisi na kuwa sasa
wazazi wake wako katika hali mbaya na yeye anasakwa hivyo ni vyema wakiachana maana anaona Maisha yake yapo hatarini pamoja na familia yake.
Binti Yule akawa akiiba fedha na kuwapelekea wazee wale ili wajikimu na baadae akamshauri Yule kijana kuwa wakimbie waende mbali wakajifiche na kuanza maisha yao wakiwa kama mme na mke.
Baada ya mabishano ya siku kadhaa Yule kijana akakubali na binti akachukua fedha nyingi za kuweza kuanza maisha popote pale watakapoamua kuishi.
Yule tajiri alipatwa na butwaa na hakuamini kama binti yake kakimbia, akaamua kuwachukua wazazi wa yule kijana na kuwafunga bila mafanikio na kuamua kuwaachia huru.
Mkewe na yule tajiri aliendelee kuhuzunika na kunung’unika kwa muda wote mpaka mmewe akaamua kutoa tangazo kwenye magazeti ya nchi ile na kusema amemsamehe mwanae hivyo arudi tu na ameafikiana nao kuwa waoane. Hivyo warudi kwa ajili ya harusi.
Taarifa zikamfikia yule kijana akiwa na mpenzi wake yule mtoto wa tajiri, kwa pamoja wakaamua kurudi na wakapokelewa na yule mzee ambaye akawaambia kuwa watafunga harusi mapema wiki itakayofuata na gharama zote zitakuwa zake na yule kijana atashirikiana na yule binti katika kusimamia mali za yule mzee.
Siku tatu baadae wakaamua waende kuandaa suti na shela kwa ajili ya harusi, waingia kwenye duka
la nguo za harusi binti alivyaa shela ikawa imemkaa safi sana na yule
kijana naye suti ilimfaya aonekanye maridadi sana,akaamua kabla ya kuvua ile nguo avuko barabara aende akanunue ice cream maana binti Yule alikuwa anapenda sana kula ice cream.
Wakati kanunua ile ice cream na anavuka barabara gari likamgonga yule kijana na yule binti baada ya kuona vile alimkimbilia na alipofika
pale damu iliruka na kutengeneza doa kwenye ile shela, wakamchukua na
kwenda nyumbani ambako baadae mazishi yalifanyika.
Baada ya mazishi binti Yule aliendelea kuhuzunika na hakutoka ndani kabisa.
Siku moja baada ya miezi kadhaa kupita usiku akiwa kalala alimtokea bibi mmoja na kumwambia katika ile shela kuna doa hivyo anatakiwa alifuo litoke au balaa litamtokea.
Yule binti kweli asubuhi aliamka na kwenda kuitazama ile shela na kukuta ina doa, akafua sana mpaka doa akaona limeoptea. Lakini alipolala tena Yule bibi akamtokea tena na kumwambia lile doa halijatakata hivyo afue tena au balaa itaikumba familia yake.
Siku ya pili akaamka na kufua lakini kila alipofua yule bibi alimtokea na kumwambia vile viele,yule binti akaona sasa kachoka ni vyema amshirikishe mama yake.
Mama yake akashangaa sana kwani naye
aliota ndoto kama ile ile na alikumwa akiogopa kuwashirikisha. Mama na
mtoto wakanya siri na kulifua tena lile shela na hata baada ya kulifua yule bibi aliwatokea tena na kuwaambia kuwa bado doa lipo.
Mmmh kazi ikawa ngumu ikabidi wamshirikishe baba, baba naye kumbe wamekuwa akitokewa na yule bibi na akawa anona sio vyema kuwashirikisha wanafamilia.
Basi baba akawaamuru waichukue ile shelana kwenda kuifukia.
Baada
ya kuifukia Yule bibi aliwatokea na kipindi hiki alikuwa mkali zaidi na
kuwaambia wana siku mbili tuu za kulifukua lile shela na kulifua mpaka
doa litakate la sivyo kuna jambo kubwa litawatokea .
Familia
nzima walilifua kwa ushirikiano na wakakubaliana kuwa sasa limetakata
na wakalianika na kulipiga pasi baada ya kukauka na uliweka sandukuni. Usiku wakiwa wamelala.waliambia wameshindwa.
Basi familia siku ya pili walikutana na kusimuliana wote wakaonyesha kuota ndoto sawa. Siku ya pili wote wakaenda kazini na kumwacha yule binti aiwa nyumbani peke yake.
Akiwa kaka peke yake na huku akisubiri mwisho wake huku akilia kwa uchungu na kumkumbuka mchumba
wake yule kijana,mara mlango ukagongwa na baada ya kumkaribisha binti
yule alistaajabu kuona ni yule yule bibi mzee ambaye amekuwa akiwatokea
usiku. Lakini mara hii alikuwa kashika kopo dogo mkononi na kumpa yule binti kasha akaondoka zake.
Je unafikiri Yule bibi kizee alimpa kopo la nini?
Jibu ni kuwa alimpa kopo la sabuni ya unga aina ya omo ambalo hutoa madoa kwa uhakika
Ha ha ha ha ha ha ha ha ni janga sana. Kama ulisoma huku ukifikiria uchawi shindwaaaaaa