
Nimechoka na kero za kila siku, sitaki kabisa yaani ni bora tu niondoke nirudi kwetu" Stara Alikuwa anazungumza kwa sauti iliyoonyesha kuwa na uchungu sana kutokana na tabia za mume wake ambaye alikuwa anachelewa kurudi nyumbani na akirudi anakuwa amelewa sana. Hali hii ilikuwa inamuumiza sana Stara ambaye alikuwa anavumilia kwasababu alikuwa anampenda mume wake.
Maisha ya Stara na mume wake kabla ya
kuingia kwenye ndoa yalikuwa ni maisha yaliyojaa furaha na upendo,
lakini baada ya kuingia kwenye ndoa mambo yalibadilika, Kutokana na hali
hiyo Stara alikuwa akiumia sana ilifikia kipindi akawa anashindwa
kuvumilia kutokana na tabia ya mume wake kumpiga, na kuna wakati
alikuwa akirudi amelewa usiku wa manane alikuwa akimlazimisha Stara
kuwa naye kimepenzi kwa nguvu hata kama Stara akisema anaumwa, yeye
alifanya nguvu yaani alikuwa akimbaka mke wake kutokana na kumtaka
kimapenzi kwa nguvu bila ya kumuandaa. Stara aliumia sana.
Na siku moja aliamua kwenda nyumbani na
kumueleza Mama yake mzazi matatizo anayokutana nayo. Mama yake
alimsikiliza kwa umakini na baadaye aliondoka na Stara hadi nyumbani kwa
mume wake ambapo siku hiyo mume wa Stara alikuwa nyumbani, Baada ya
Mama kuanza kumuuliza maswali kwanini anamtesa Stara. Mwanaume huyo
alikuwa amenyamaza kimya huku akionekana kuwa mpole kana kwamba
anaonewa, "Sikiliza nikuambie kijana, chonde chonde naokuomba
usiniumizie mtoto wangu, kwani sintojali kama wewe ni mkwe wangu,
nitakupeleka polisi, na tena jambo hili sijamfahamisha Baba Stara, sasa
mimi naondoka lakini nakuambia kama mtoto wangu umemchoka ni bora
umrudishe nyumbani kuliko kumpiga kama ngoma."
Aliongea Mama Stara huku akionekana
kuwa na hasira. Mume wa Stara aliomba msamaha na kuahidi kuwa hatorudia
tena. Baada ya siku mbili kupita tokea Mama Stara aende kuwasuluhisha
pale nyumbani.
Siku hiyo Mume wa Stara alikuja
nyumbani kama kawaida akiwa amelewa sana, alianza kumtolea maneno
machafu mke wake "Wewe mwendawazimu, njoo hapa, nimekuambia sogea hapa"
Stara alikuwa anatetemeka huku akisema "Lakini mume wangu si ulisema
umeacha pombe, na hautonipiga tena" Kabla hajamaliza kuongea alivutwa
kwa nguvu na kuanza kupigwa vibao katika paji la uso wake, alilia na
kulalama kwa uchungu "Mimi siwezi kabisa haya maisha, nimechoka, sitaki
mimi, kila siku unanipiga, nimekukosea nini mimi, naondoka narudi kwetu,
nimekuchoka sikutaki niachie unaniumiza".
Aliendelea kumpiga bila ya huruma huku
akisema "Siwezi kukuacha wewe ni wa kwangu tu, na utakufa na mimi"
Stara alikuwa anaogopa alijivuta kutoka kwenye mikono ya mume wake na
kukimbia huku mume wake akimkimbiza. Kwa bahati nzuri alikutana na
taksi akapanda haraka na kuelekea nyumbani Baba na Mama yake walipomuona
walihuzunika sana na moja kwa moja walipiga simu polisi na Mume wa
Stara alikamatwa na kwenda kufunguliwa mashtaka ya kumpiga mke wake.
Stara alirudi nyumbani kwao na kuamua
kuishi na wazazi wake. Mume wake aliachiwa huru, baada ya kulipa faini,
lakini bado anaendelea kumsumbua Stara na kumtumia ujumbe kuwa
"Anampenda na kamwe hawezi kumuacha" Lakini Stara ameamua kuendelea na
maisha yake. Huku akiwa makini na kutakiwa kutoa taarifa polisi endapo
kama atafanyiwa jambo lolote na aliyekuwa mume wake.
NI VYEMA KUTOA TAARIFA ILI USAIDIWE INAPOTOKEA UNAFANYIWA UKATILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni