Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo
haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo
zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio
ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye
sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya
Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu.
Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake
kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa
kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile,
akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa
ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma.
Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia
kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa
‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia
vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika
mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka
kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya.
Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na
mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu
mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda
kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya
mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao
wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo
mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale.
Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha
kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla
nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo
lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule,
nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa
umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea
kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa
aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi
tulipomaliza bado alisimamia msimamo.
Sasa nikajikuta katika pepo mbaya,
nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi
lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti
huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini
siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo
haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa
marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!!
Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu.
Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye
naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika
nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima
yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi.
Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa
nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu,
niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake
sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile
kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe
sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa
macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka
mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo,
nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara
akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli
sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile
“ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa,
na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema, binti
akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria
wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu.
Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na
kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa
nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na
niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada
ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu.
Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE
baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu
ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa
maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa
mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda
uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa
naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba
yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi
hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji
iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako
haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari
kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi
lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala
usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa
mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake.
Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi
ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu
…nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa
nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi
kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni
heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu
ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama
ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa
kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu,
nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na
mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili
siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta
napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya
kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini
ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani
kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine
dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi
aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau
mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na
hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE
MTUMWA!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni