Alhamisi, 28 Mei 2015

NILIMTAFUTA MIAKA SITA


  Nakumbuka ilikuwa ni siku ya alhamisi nilipokutana naye kwa mara ya kwanza.Siku hiyo nilikuwa shuleni,alipokuja shuleni kwetu.
Nilikuwa nje nikimalizia muda wa mapumziko,niliegemea kwenye nguzo ya nje ya darasa letu,nimeinama nikiwaza juu ya ombi la John la kuwa naye kimahusiano ya kimapenzi aliloniambia jana.
            Nilipoinua kichwa changu nilimwona mvulana mgeni katika macho yangu, mrefu na mwenye mwili mwembamba,alikuwa amependeza sana.Si kwamba alivaa vipi ,ni jinsi ya rangi ya bluu na fulana nyekundu,ndiyo iliyomfanya aonekane simati na kunitoa udenda.
Alipozidi kusogea karibu na kuonekana barabara  mapigo ya moyo yalibadilika nikaona yanaanza kwenda mbio mbio.Mfumo wangu wa damu ulibadilika,damu ikaanza kwenda kwa kasi zaidi.
Ni upendo mkubwa uliojitokeza baada ya kuonana na Krisi,moyo wangu ulivutiwa sana na mwonekano wake tu,ingawa sikuwa namfahamu tabia yake na hata jina ,sikulifahamu ,lakini hayo yote hayakuwa na nafasi katika fikra zangu.
Nilimtazama sana macho yangu yalikuwa kama yamepigwa na shoti ya umeme kwani yaligeukia huko yakaganda kumtazama.Nilitamani aniongereshe ingawa sikuwa na  uhakika kama angeweza kufanya hivyo.
Nikiwa bado nafikiria na kumungoja ili nione kama atapita nilipokuwa nimesimama,Yule kijana alizidi kusogea karibu yangu.
Moyoni nikawa namshukuru Mungu, nikimwomba japo yule kijana aseme neno moja tu.
’’Anti mambo,antii mambo’’  ni salamu  ya Krisi nikiwa kama niko usingizini au nimezimia,hivyo nimesituliwa ,nikamjibu kwa kusituka  ‘’mh! salama’’.
 ’’Eti unamfahamu Juma anayesoma Kidato cha nne’’  aliniuliza swali,nikamjibu kwa kutafakari kwanza ni Juma yupi,nikamwuliza Yule Juma  bonge bonge anayesoma kidato cha nne B?
Naye akasema  ‘’ndiye huyo,ninaweza nikamwona ,mimi ni kaka yake nimekuja kumtembelea? ‘’Nilimwomba anisubirie kidogo ili nikamwangalie,kama atakuwemo darasani.
Bahati nzuri nilipoenda nikakuta darasa limetulia utazania wote walikuwa wamesinzia,kila mtu akipekua daftari lake na kumsubiria mwalimu,nikauliza kwa nguvu kwa kutanguliza kuomba radhi kwa usumbufu,
 ‘’ Eti juma yupo, kuna ndugu yake anamtafuta, yuko pale nje?”.
Juma akajitokeza  ‘’yuko wapi huyo ndugu yangu”.Macho yote yakageukia kwa Juma,watu wakafunika daftari zao na kumtazama yeye.Juma aliinuka kwenye kiti chake akanifuata, nikwamongoza tukaenda pale alipokuwa amesimama Krisi.
’’ Aah vipi Krisi ,karibu sana kaka’’ Juma akimkaribisha Krisi huku akimsogelea na kumkumbatia,
Krisi naye alijibu,
“nashukuru sana kaka”
“kiskani vipi mwanangu?”
  ‘’ Poa tu wote, ni wazima,wanakupa hai tu”
Baada ya kumaliza kusalimiana ,mimi nikiwa nimesimama nikiwasikiliza tu,nijue nini kitakachoendelea,Juma alimwambia Krisi amsubirie akachukue daftari zake ili waondoke.
Krisi akajibu ‘’ hamna noma utanikuta nakusubiri.’’
   Sasa tukabaki mimi na yeye,nikavuta pumzi ,nikijiuliza namna ya kumuanza,na mimi ni msichana ,nikimwambia ai lavu yuu ataniona mimi kicheche,kwa maana ni mara ya kwanza kuonana naye na mimi ni msichana.Maswali yakazidi kuzunguka katika ubongo wangu wa mbele,huku ukimya ukiwa umetawala.
‘’anti nashukuru sana kwa kunisaidia” haya ni maneno ya Krisi baada ya muda kama wa dakika mbili ya ukimya akinishukuru.
 ‘’Hamna shida kaka kawaida tu ‘’ nikaona hii ndiyo nafasi ya kuitumia ,nikiwa na falsafa ya kimichezo inayosema “one chance one goal” yaani ikimanisha “nafasi moja ,goli moja” nikamuuliza ,
’’ eti kaka unatokea wapi?”
   ‘’natokea igoma’’ .Nikamwuliza swali lingine  “unasoma?’’
 ‘’ee mimi ni mwanafunzi wa arusha teki”.
Sikuishia hapo nikamuuliza habari za masomo,
‘’ masomo yako freshi tunakomaa mdogo mdogo’’
Hata hivyo yeye alionekana kutotaka kujua habari zangu kabisa kwani hakuniuliza lolote kuhusu mimi masomo au habari za hapa shuleni.
Nilipoishiwa maswali nikanyamaza ndipo ukimya ukatanda tena kabla hajaja Juma.Lakini baada kama ya dakika mbili nikasikia akiniuliza ,
  ‘’hivi wewe anti jina lako nani”
Kwa haraka haraka nikamjibu,nikajiseme amoyoni haya ndiyo niliyokuwa nayasubiria ‘’ naitwa Aneth John”.
Ingawa tayari nilikuwa nimesikia kuwa anaitwa Krisi  nikaona nimuulize nione mwitikio wake  ’’ naitwa Krisi’’. Ndipo nikaanza kumsifia ‘’aah jina zuri sana’’.
 Akionyesha tabasamu akasema ’’asante! hata wewe una jina zuri’’.
  Hii ikamfanya afunguke,na kuanza kuniuliza maswali mbalimbali.
  “walimu vipi hapa”
‘’ kwa  kweli walimu ni tatizo hasa mwalimu wa fizikia na hesabu hatuna kabisa,huwa wanaletwa tu kutoka shule mbalimbali kutuelekeza kwa wiki moja katika mwezi mmoja’’
    ‘’ poleni sana,hapa inabidi ukifunga ukasome tuition tu, kama unataka ufaulu vizuri masomo hayo”
 “huwa tunafanya hivyo”
Akazidi kuuliza ‘’ kwa hiyo wewe unaishi kwenu au na wewe umepanga?’’
‘’mimi ninaishi nyumbani,wazazi wangu wanakaa hapa hapa ”.Tukiwa  tunaendelea, juma akaaja
  ‘’twende kaka”
             Basi Krisi akaniaga ‘’aneth nashukuru sana tutaonana Mungu akipenda”
  Niliumia sana moyoni kwani nilikuwa nimeanza kupata faraja kubwa.Ile tu kuongea naye ,nilikuwa najisikia kama kwamba tayari alikuwa amekuwa wangu.
            Nilitaka kushindwa kumjibu ,nikajilazimisha ili nisionekane kuwa tayari nilikuwa nimezimika niilimjibu kwa unyonge ‘’ poa safari njema”
             Juma aliponiona najibu kwa unyonge akahisi kitu ,akaniambia
‘’ hata hivyo atakuwepo geto njoo mpige pige stori kabla hajarudi sikani “.
             Moyo wangu uliripuka furaha, ingawa sikuonyesha kuwa nimefurahi kiasi hicho,nikajifanya kama sina uhitaji sana,nikamwambia Juma ‘’nitacheki kama nikipata muda nitakuja”
‘’powaa baadaye”
Waliniacha wakaondoka,mimi nikabaki kumalizia muda wa kuwa shuleni siku hiyo uliokuwa unaisha saa nane na nusu.Yalikuwa yamesalia kama masaa matatu,tutakapotawanyika kurudi nyumbani.
Baada ya kuondoka kiukweli , sikuwa tena shuleni wala darasani akili yangu yote nilikuwa namfikiria Krisi.
Ni mwanaume niliyekutana naye mara moja lakini alifanikiwa kwa asilimia kubwa kuteka sehemu kubwa  ya moyo na akili yangu.Kila nikimwangalia katika macho ya akili yangu mwili wote ulisisimuka.
Kila mwalimu aliyeingia darasani kufundisha alinitambua kuwa siko sawa kwani sikuwa nimechangamuka hata kidogo ila nilionekana kama niko kwenye dimbwi la mawazo.
  “unawaza nini aneth leo mbona unaonekana hauko sawa?” mwalimu mmoja wa Kiswahili aliniuliza.
“mbona  nipo sawa mwalimu”
‘’uko sawa wewe,mbona tangu niingie umeinama tu unaelewa ninachokifundisha kweli?”
Nikaa kimya sikujibu lolote.Alipoona hivyo hakutaka kunifuatilia sana akaendelea kufundisha,nami nikaendelea kuweka mawazo yangu kwa Krisi nakuweka kando swala la kumsikiliza mwalimu.
Nilihisi siku hiyo muda ulikuwa hausongi mbele kama inavyokuwa kwani nilitamani ufike mapema ,tutawanyike ili mimi niende nikaoanane na Krisi getoni kwa Juma.
Nikawa namwoma Mungu ayakimbize masaa ili muda wa kutowanyika ufike ,ili niende nikamwone tena Krisi
Nilimwomba pia Mungu anisaidie ili atambue nini ninachokiwaza moyoni mwangu.Tunajua sote kuwa kwa mwanamke kumuanza mwanaume ni vigumu sana ingawa inawezekana.Nikiwa katika kuwaza hivyo nilijikuta nimepitiwa usingizi.
Usingizi ulinoga sana siku hiyo na bahati nzuri mwalimu wa somo la histori hakuwepo siku hiyo kwa hiyo hakukuwa na kipindi darasani,nilichapa usingizi kama li saa moja hivi.Nikiwa ndotoni mawazo yangu yalielea kumuota Krisi  tu,nilimwona kama tuko pamoja tunaeleka katika sayari Fulani ya mapenzi.
Tukiwa hewani tunaelea ,tuliongea kwa furaha huku tukikumbatiana,pigana busu na kuzama katika mahaba mazito.
Nikaja kusituka pale niliposikia ninaamushwa,kwaa kuwa jina la Krisi ndilo lililokuwa limetawala sehemu kubwa ya ubongo wangu wa mbele nilijikuta naitika “naamu Krisi” akili yangu iliporejea katika mfumo wake wa kawaida nikagundua kuwa hakuwa Krisi bali alikuwa mwanafunzi mwenzangu alikuwa akiniamsha baada ya  kengele ya kutawanyika kwenda nyumbani  kugongwa na mimi nilikuwa naendelea kufaidi usingizi.
Niliamuka,nikajifuta macho yangu kwa leso yangu kuondoa tongo tongo,nikijinyosha nyosha mikono na shingo,huku nikipiga miayo.
Nikakusanya madafutari yangu huku nikimshukuru julieth kwa kuniamsha.
‘’hamna shida,lakini mbona unaniita Krisi au Krisi wa wapi?”
  ‘’ndoto za usingizini tu hizo,hamna shida”
  ‘’ok{sawa) fanya haraka tuwahi paredi”
  ‘’haya ngoja nichukue sweta langu tuondoke’’
Tulienda paredi,tukafika tukajipanga kwenye mstari.Mwalimu alikuja akatoa matangazo kisha akatutowanyisha.
Kwa kuwa nilikuwa ninaenda kwa kina Juma ilibidi nimuarifu mdogo wangu Pendo ili akawape taarifa wazazi watakapohoji kwamba nimeenda wapi.
Nilimwambia mama akikimuuliza amwambie tu kwamba nimebaki shuleni mwalimu ametuambia tubaki ili tufanye prakitiko.
Alikubali ila akaniuliza swali ‘’kwani dada unaenda wapi kiukweli?”
   ‘’wew nenda nikirudi nitakuja nikwambie” nilimwambia hivyo huku nikiondoka kuelekea kwa kina Juma.
Sikuwa nimefika alipokuwa anaishi Juma kwa hiyo ilibidi niende na mwanafunzi mmoja aliyepanga nyumba moja na akina Juma.
Baada ya dakika chache tukawa tumefika kwani walipanga karibu na shule.yule dada akanionyesha  mlango wa chumba cha akina Juma,yeye akaingia kwenye chumba chake.
 Nikamshukuru kisha nikasogea mlangoni nikapiga hodi
  ‘’karibu”
‘’hodi mpaka ndani”
‘’ingia tu hapa ni geto”
Nikafungua mlango uliokuwa umeegeshwa na kuacha viatu vyangu mlangoni.
 “ingia tu na viatu ,wewe usihanye”
“nashukuru,nilikuwa nimeshavua kwania kuna mtu anaweza kuja kuchukua?”
  “hamna mwizi mitaa yetu hii”
Niliingia ndani nikakaribishwa kukaa kwenye,situri.
            Krisi yeye alikuwa amejilaza kwenye godoro,nilipofika akainuka,na kunikaribisha,
“karibu miss aneth ,hapa ni kwetu sote” Alionekana kuwa ni kijana mtaratibu, mstarabu na mwenye moyo wa kujali, kitu ambacho kiliongeza kumpenda zaidi.Alinijali sana ,aliagiza soda na keki mbili kwa ajili yangu ,huku tukisubiria pia chipusi mayai ambayo aliagiza nitengenezewe kwasababu wao walikuwa wamemaliza kula.
Alitambua kuwa nimetoka shuleni nimechoka na nina njaa ndiyo maana akatafuta chakula ili tuweze kuongea vizuri kwa maana ukiwa na njaa hata kuongea unaweza kushindwa.
Kwa kweli kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo nilivyozidi kudata kwa Krisi,alinichanganya sana kiasi cha kufukia kushindwa hata kuongea.
Niliingiwa na usingizi wa mahaba,nikainuka pale kwenye situri nikajilaza,alipokuwa Krisi kwa kisingizio kuwa naanza kujisikia vibaya,kichwa kilikuwa kinanigonga.
Krisi alienda kumuita Juma na kumpa hela akanichukulie dawa za kichwa kisha akarejea ndani na kunituliza,
“usihofu Aneth utapona,nimemtuma Juma ameenda kukuchukulia dawa”.
“Asante,ila usingehangaika hivyo kwani nadhani ni uchovu tu”.
“usijali uhai,ndiyo kitu cha muhimu kwa mwanadamu”.
Nilianza kumlaumu moyoni,ina maana hajaelewa kuwa haya ni mapozi tu?
Alichukua shuka akanifunika kiwiliwili akaniambia,nikute nimepumzika nikisubiria dawa.
Nilivuta shuka nikajifanya niko siliazi nimelala,kumbe mawazo yote yako kumuwaza Krisi.Baada ya muda mfupi Krisi aliniamsha kwa kunipapasa miguu na vidole vyangu vya miguu,akiniambia niamke ninywe dawa.
Kulingana na raha niliyokuwa naipata,niliekiti nimesinzia ili aendelee kuishika shika miguu yangu.
Alipoona siamki aliniacha niendelee kulala,nitakunywa nitakapoamka.
“dada naona alikuwa amechoka,umemwamsha hivyo hata hajielewi”  nilimsikia Juma akimwambia Krisi,
“inawezekana,ngoja tumwache apumzike”.
Baada ya kumaliza kusema hivyo,Krisi alianza kuangalia picha za Juma zilizokuwa kwenye Albamu,Juma yeye alichukua daftari akaanza kujisomea.
Krisi alipomaliza kuangalia picha alisogea karibu na kichwa changu ,kisha akaanza kunipapasa papasa hasa kwenye kichogo au pale medulla obulongata hukaa.
Uzalendo ulinishinda ,ikabidi niamke nimwambie laivu kuwa nampenda.
Alipoona nimeamuka aliondoa haraka haraka mkono wake kwenye kichwa changu.Nijishosha kana kwamba nilikuwa kwenye usingizi mzito.
“Vipi kichwa,kinaendeleaje?”
“afadhari ,kimepunguza maumivu”
“pole”
“asante”
“tumekuletea dawa,hii hapa” alinipa
Nikaipokea tu ili nisimhuzunishe kwa kuona kwamba amefanya kazi bure lakini sikunywa niliiweka mfukoni nikamwongopea kuwa nitaenda kunywa nikifika nyumbani.
Nilinyanyuka pale kitandani nikajiandaa kwenda nyumbani,kwani usiku ulikuwa umekaribia kufika.
Niliamuka nikanawa uso,nikajifuta na kujipaka mafuta ya baby care niliyoyakuta pale .kisha nikamwomba Krisi anisindikize.
“si ungelalala huku tu”
Krisi alinitania
“aa,hapa nitalala wapi?”
“si humo ,tunalala wote”
“subutuu..”
Niliposema hivyo akanishika mkono wangu akiniambia tuondoke asije mama akaja kunitafuta.
   Tulianza safari kuelekea nyumbani,huku Krisi akiwa amenishika mkono wangu wa kushoto.
   Tukiwa njiani,yeye mwenyewe Krisi alijiingiza kwenye kumi na mbili zangu,baada ya kuniuliza kama ninampenzi ama mchumba?nikagunduamkuwa na yeye alikuwa ameanza kunizimia.
   Sikutaka kuvunga kuwa ninaye kwani niliogopa kuwa angeweza kukata tamaa,ikabidid nimwambie ukweli kuwa sinaye.
    “je akijitokeza sasa hivi mtu akakuomba awe mchumba wako,utakuwa na maamzi gani?”
“nitamwangalia,na mchumba mwenyewe,kama nikimwona anafaa,nitakubali”
“kwani unahitaji awe na sifa gani”
Nilianza kuporomosha sifa nyingi ambazo yeye alikuwa nazo zote.Akaniuliza kama sifa hizo yeye alikuwa nazo.
  “unazo” nikajiweka kwenye ndoano mwenyewe,bila taabu.Niliposema hivyo alinitazama usoni,akanisimamisha,kwani tulikuwa sehemu ambayo watu hawakuwepo njiani,alikanishika shingoni,na mimi nikamshika kiunoni,tayari tukaingia sayari nyingine kwa sekunde chache sana kwasababu ilikuwa njiani.
                        Kila mmoja aliramba mdomo na ulimi wa mwenzake,na kupigana busu nyingi nyingi kisha tukaendelea na safari kwa sababu kuna watu walikuwa wanakuja mbele yetu.
            Krisi alinieleza kuwa ananipenda sana,ingawa hajanifahamu vizuri lakini aliniona kuwa ninafaa kuwa naye kimapenzi.Kwa hiyo sote tulipendana,kwani mimi nilifikiri kuwa ninampenda mimi tu ,nikashangaa kuona kuwa na yeye alikuwa ameshanipenda.
  Hivyo ndivyo safari yetu ya mapenzi ilianza,tulipokaribia nyumbani Krisi aliniaga kuwa hataweza kufika nyumbani,anaogopa wazazi wangu.Mimi nilimlazimisha tukafika mpaka nyumbani.
            Nilimkuta mama anaandaa chakula cha jioni,tulimsalimia mama.Baada ya salama nikamtambulisha Krisi kwa mama kuwa alikuwa mwanafunzi mwenzangu,akamkaribisha.
            Tuliingia ndani,nikamkaribisha Krisi kwenye kochi,akakaa,mimi nikaenda kubadilisha nguo,nikavua nguo za shule na kuvaa nguo za nyumbani.
  Baada ya kumaliza kuvaa,nilikuja sebuleni alipo asali wangu wa moyo.Aliniomba maji ya kunywa,nikampa.
 Nilipokaa akaniomba kuwa anataka kurudi nyumbani ,kwasababu giza la saa moja lilikuwa limeanza kuingia.
            Nilimkubali, tukaenda kumuaga mama.Mama alimwomba Krisi asubiri chakula ,lakini hakukubali  kwa kudai kuwa anawahi,atakuja siku nyingine kula.
            Tuliondoka,nikamsindikiza Krisi.Nilienda naye mpaka sehemu moja hivi ambapo kuna nyumba ilikuwa inajengwa na hakukuwa na watu kwenye nyumba jirani  ambayo nayo ilikuwa inafanyiwa finishingi,hivyo hawakuwa wamehamia.Tuliingia ndani ya nyumba hiyo tukakaa na  kuanza kupiga stori.
            Nilikaa kwenye mapaja ya Krisi, tukiendelea kupiga stori,za kufahamiana zaidi,huku akizungusha mikono na vidole vyake katika sehemu mbalimbali za mwili wangu.Alikuwa fundi wa kucheze sehemu mbalimbali za mwili wangu,akizungusha mikono yake kwenye tenesi zangu,kiuno na uti wa mgongo wangu.
Alivyokuwa akinishika shika ilinifanya nishindwe kuendelea na stori,nilizidiwa sana kwa jinsi alivyokuwa akitembea katika sehemu zangu nyeti.Nilijiachia nikalala kwenye nyasi zilizokuwemo ndani.Krisi akakaa juu yangu kwenye kiuno changu ,akanifunua kwenye tumbo langu akaanza kuramba kitovu changu huku akielekea kwenye kifua changu.Hali hii ilinifanya nizidi kuchanganyikiwa kuanza kutetemeka.Nikamshika kwa nguvu Krisi,hata hivyo alishtuka akashuka juu yangu ,nikamshikiria lakini akaniomba sana tusifanye siku hiyo.nilimlaumu kwa kuniandaa kimchezo harafu akaahirisha mechi,wakati  huo tayari nilikuwa nimimeingia katika  hali ya mchezo,kuahirisha mchezo iliniumiza sana.
            Hakutaka tucheze mechi  siku hiyo kwa kuwa hatukuwa na Mwamvuli na tulikuwa bado hatujazoeana.
Aliniaga ,akaondoka na mimi nikarejea nyumbani huku jasho la mazoezi tuliyofanya likiwa linanitoka.Nilienda nakimbia ili nimuwahi baba kabla hajarudi toka kazini, saa mbili.
            Nilimkuta mama ameshaivisha chakula,nikaenda kwanza kuoga kabla ya kula.Nilipomaliza kuoga, mdogo wangu pendo alitenga chakula,tukala.
Baada ya kula nilienda kitandani kulala.Sikutaka kuangalia hata muvi ya siku hiyo,kwani nilikuwa nimechoka sana na akili yangu haikuwa sawa .Hata kujisomea nisingeweza kwani mawazo yangu yote yalikuwa kwa Krisi.
            Baba alipokuja aliniulizia akaambiwa nimelala.Pendo akatumwa kuja kuniita.Nilienda ,akaniuliza kwanini ninalala mapema sana siku hiyo ama nilikuwa naumwa?
            Nilimwambia baba kuwa nilikuwa nimechoka tu,kwa kuwa nilikuwa nimeshinda shuleni.
            Akaniruhusu kwenda kulala,nikaenda kulala.
Usingizi ulipaa kabisa,akili yangu ilikuwa ikizunguka katika  kumuwaza Krisi,nilikumbuka jinsi alivyonifanyia kwenye nyumba ile.Nilikumbuka soda na keki,chipsi na jinsi alivyonijali pia kwa kwenda kuninulia dawa baada ya kuona kuwa naumwa.
Nikajisemea moyoni kuwa yule ndiye anafaa  ndiye anafaa  kuwa mwenzi wangu wa maisha,na hili ndilo chaguo la Mungu kwangu kuwa awe wangu wa maisha.
            Nilikumbuka hata kitendo chake cha kukataa kufanya kitendo cha wakubwa cha usiku,nikatambua kuwa si mwanaume mpenda uasherati,kwani angekuwa mpenda kufunga magoli asingekubali kuacha kufunga, kwa kuwa tayari nilikuwa nimeliacha goli wazi ili afunge.
            Nikiwa katika kumwaza mahabuba wangu wa mtima wange,nilimsikia mama yangu akiniita kwa nguvu ,nikanyanyuka nikamfuata,akanipa simu kwa kuniambia ni simu ya mwalimu wangu.
            Nilipoipokee  nikagundua ya kuwa alikuwa Ni Krisi alijifanya kuwa ni mwalimu wangu,hivyo ananiomba nije na kitabu chake kesho.Alitaka kunijulisha kuwa amefika salama,na kunitakia usiku mwema.
            Hatukuweza kuongea sana kwasababu mama alikuwa amesimama akisubiria simu yake aende kulala.
Nilikubali tu nakumjibu kwa kifupi kisha nikata simu asije mama akashtukia dili.Nilimpa mama simu yake nikamshukuru.Baada ya kuipokea akaniuliza habari za Krisi kama nilikuwa ninamahusiano naye ya kimapenzi,nikakana.Mama alianza kusifia uzuri wa Krisi na unadhifu wake.
Akaniuliza kuwa   anakaa wapi yeye,sikumwambia kuwa alikuwa mgeni kwa hofu kuwa angegundua kuwa nilikuwa nina uhusiano naye kwani isingewezekana mgeni tu awe rafiki yangu nimlete mpaka nyumbani bila mahusiano ya kimapenzi,nikamwambia kuwa alikuwa anaishi sehemu ambayo Juma ,nduguye alikuwa akiishi.Akanijibu sawa.Nilimuaga mama kuwa naelekea kulala,nikaondoka.
             Nilimwacha mama akiwa amesimama huku akionekana kama alikuwa akifikiria inshu Fulani nikataka nimwambie ukweli, lakini moyo wangu uligoma nikaogopa kuwa huenda mama alikuwa ananitega.
              Nilirudi kulala ,usiku karibu wote nilikuwa na mwaza Krisi,nikilala na nikiamka.Kwa sehemu kubwa alifanikiwa kuiteka akili na mawazo yangu,nilishindwa hata kusoma katika usiku ule.Tulikuwa na kawaida ya kuamuka saa tisa,mama alikuwa anatuamsha ili tujisomee na kujiandaa kwenda shuleni,lakini siku hiyo sikuweza kuamka .Mama alijaribu kuniamsha mara nyingi lakini sikuweza kuamka.Baba akamkataza asiendelee kuniamsha huenda nilikuwa sijisikii vizuri.
            Nilipoamka saa kumi na mbili asubuhi,mama aliniuliza kama nilikuwa naumwa kwasababu aliniamsha sikutaka kuamka,nikamwongopea kuwa nilikuwa najisikia vibaya.Kichwa kilikuwa kizito lakini sasa hivi najisikia vizuri.
            Nikaenda kuoga,nikamaliza nikavaa nguo za shule ,nikaanza kwenda shuleni.
Nilienda moja kwa moja hadi kwa kina Juma ili nikaonane na Krisi.Niliwakuta bado wamelala.Niliwagongea ,Juma akaja kunifungulia , alishituka aliponiona,akarudi ndani.Akaenda kuvaa fulana,kwani alikuwa amevaa pensi tu hapo mwanzo.
            Nilimuuliza, Krisi hajaamka?
“bado,alichelewa sana kulala jana?”
“hawezi kuamka?
“Labda nijaribu kumwamsha” aliingia ndani akaenda kumuamusha Krisi akimweleza kuwa kuna mgeni wake nje.
“mgeni  gani au aneth?”
“nani mwingine zaidi ya huyo?”
“mwambie anisubiri hapo nje”
Alikuja nje akaniapa situri ,nikakaa.
Baada ya muda mfupi Krisi alikuja ,akanikaribisha.
“asante”
“za tangia jana”
“nzuri tu”
“vipi ulimuwahi mzee?”
“ee,nilipofika ,nikakaa kidogo na yeye akaja”
“du! Kwa hiyo ungechelewa kidogo tu ,ingekuwa baraa”
“mzee yule alivyo hataki kutuona saa mbili hatuja fika nyumbani,sijui ningemdanganyaje? Yeye anataka akirudi kutoka kazini awakute wote.Asipowakuta atauliza mno fulani kaenda wapi?”
“haha haha, inaonesha mzee anawapenda sana”
“kusema ukweli baba anatujali sana”
“ok !ngoja ninawe uso basi nikusindikize”
“poa fanya fasta  kwa maana ,taimu limeenda”
“poa”
Aliondoka akaenda kunawa uso ,akaniacha nimekaa nje,huku nikiangalia simu yake aliyoniachia.
Baada ya muda mfupi alikuja yule dada aliyenileta hapa jana,akitokea chumbani mwake.Nikahofu kidogo kuwa  tayari naenda kuumbuka ila nilijiamini kwa kuwa yeye alikuwa anasoma kidato cha pili asingeweza kuvumisha habari zangu masikonga.
“vipi aneth?”
“poa tu,naona unatangulia?”
“ee,vipi wewe  tusepe”
“tangulia nitakukuta”
“poa  basi mimi natangulia”
“hayaa”
Baada ya sethi kuondoka,nilikaa muda kidogo Krisi alikuja,alikuwa amevaa nguo nyingine mbali na zile za jana ,alipendeza kweli kweli,nikaanza kujisifu moyoni kumpata mwanaume nazifu kiasi hicho.Nikamuuliza kama tayari ili tuanze safari,akasema yuko tayari tuanze safari,tukaondoka.Tukiwa njiani Krisi aliniongeresha,
“leta habari sasa Aneth”
“mimi niko byee ,sijui wewe?”
“hata mimi niko safi”
“basi vizuri”
“ila leo mimi naondoka”
“ee unarudi nyumbani,kwanini usingeenda kesho?”
“hata mimi nilikuwa nimepanga hivyo ila mzee kakomaa nirudi leo”
“kwaa hiyo utaondoka saa ngapi?”
“saa nne”
“kama ni saa nne nisubirie saa sita ili nije nikusindikize kwa maana leo ni siku fupi”
“sawa mimi nitakusubiria”
“Asante”
Tulitembea kidogo tukipiga sitori za kuhusu masomo,Krisi akaniaga,
“ngoja mimi nikuache”
“nashukuru kwa kunisindikiza”
“haya, masomo mema”
“nashukuru na wewe pia siku njema”
“nakupenda”
“na mimi nakupenda sana Krisi” niliongea kwa sauti ya kimahaba.
Nilimwacha, nikawahi  shuleni kwani tayari muda ulikuwa umekaribia kuisha wa kufanya usafi asubuhi na eneo langu lilikuwa chafu.
            Nilijitahidi kutembea kwa kasi ili nifike nifanye usafi eneo langu kabla ya muda wa usafi haujaisha.Nikafika nikaweka begi langu darasani ,kisha nikaenda kuchukua mfagio.Nilipopata ufagio ,nilienda kwenye eneo langu la usafi ,nikafika ,nikaanza kufanya usafi.
            Wakati naendelea kufanya usafi,John alikuja pale nilipokuwa nafanya usafi
“mambo aneth”  John alinisalimia,
“poa “  
“buku vipi?”
“safi tu”
Nilipomjibu hivyo aliomba ufagio wangu ili anisaidie,nikampa nikiwa namshukuru.
Akanza kufagia mimi nikiwa nimesismama.Baadaye akaniuliza juu ya ombi lake la kuwa mpenzi wake aliloniambia juzi.
“mimi tayari na nina mtu,tunapendana sana ,jaribu kwingine”
“lakini Aneth ujue mimi nakupenda sana,ninateseka kwa ajiri yako”
“hata mimi najua unanipenda lakini tayari mimi na ninamtu ninayempenda na yete ananipenda”
Aliendelea kunishawishi nilikubali ombi lake,nikaamua kunyamaza kimya ili aendelee kunisaidia  kufagia ,mimi niachane naye,kwani mimi mawazo yangu yalikuwa kwa Krisi.
            Alipoona amegonga mwamba,alitupa ufagio wangu akaondoka kimya kimya akionekana mwenye sura ya kunyong’onyea.Hata hivyo alikuwa amemaliza kufagia eneo langu lote ambalo nilikuwa nafanya usafi.Nikazoa takataka ,nikaenda kuzitupa kwenye shimo la taka.
            Baadaye nilienda paredi.Tukaimba wimbo wa taifa na wa shule.Tulipomaliza ,Mwalimu wa zamu aliwaadhibu wale ambao hawakufanya usafi,walioandikwa majina yao.Baadaye tuliruhusiwa  tukaenda darasani.
            Siku hiyo nilikuwa nimechangamka sana,kwa sababu ya Krisi,niliona masaa yalikuwa yanaondoka haraka sana.Kila mwalimu aliyekuja  nilijitahidi kumsikiliza vizuri na kuuliza maswali sehemu ambayo sikuelewa .Wanafunzi wenzangu wakashangaa sana,kwani si kawaida yangu.
            Muda wa mapumziko ulifika,tulitoka tukaenda kunywa chai kantini.Tulipotoka nje twende kunywa chai,nikiwa na rafiki yangu Perepetua nilishangaa kumwona Krisi akija, tena karibu na darasa langu.
            Nilienda kumpokea ,tukasarimiana,na kumtambulisha rafiki yangu Perepetua kwa Krisi.Krisi alifurahi kumfahamu Perepetua.
            Akaniambia amekuja kunichukua tukanywe chai getoni kwao ,ili  tuagane aende nyumbani.
            Nilimuaga perepetua , nikaongozana na krisi,hadi nyumbani kwao.Nilimwacha Perepetua akiwa anatumezea mate kwa jinsi tulivyokuwa tukionekana tulipokuwa tukitembea pamoja .Sikutaka kwenda na peereptua kwa sababu ya kuhofia kukosa uhuru wa kuinjoi na Krisi.
            Tulifika nyumbani kwa Juma ,tukamkuta yuko ndani.Tulipiga hodi akatukaribisha,nasi tukaingia wote,Krisi akiwa amenishika kiuno  changu.Tukakaa wote kwenye godoro.Krisi akanilalia kwenye mapaja yangu.
            Juma akatenga chai,ilikuwa ni chapati za mayai na chai ya maziwa.Krisi akainua kichwa chake,akanikaribisha chai.Tuliamuka Juma akatunawisha ,tukanywa chai.
            Tulipomaliza kunywa chai ,Krisi akaenda kuoga, tayari kwa kuanza safari ya kurudi kwao Igoma.Alipomaliza kuoga alibadilisha nguo alizokuwa nazo,alivaa nguo nyingine si zile za asubuhi,na zenyewe zilimtoa sana.
Juma akachukua begi lake,nikamwomba nilibebe akanipa, tukaanza kumsindikliza kwenda kivukoni Kamanga.
            Tulimsindikiza hadi sehemu moja iliyoitwa chemagati Juma akaomba kutuacha tuendelee yeye arudi  nyumbani.Waliagana kwa kukumbatiana ,Juma akamshukuru sana Krisi kwa kuja kumtembelea na kumtakia safari moja.Krisi alimshukuru Juma kwa kila alichomfanyia na kumtakia masomo mema.
            Mimi niliendelea naye,tukapeana ahadi nyingi za kwamba tusisaritiane.Akaniahadi kuwa ataendelea kunipenda mpaka anaingia kaburini, ,hatanisariti na atakuwa anakuja kunitembelea.Mimi pia nilimwahidi sitaigia kwenye dimba kucheza mpira na mwanaume mwingine zaidi yake.
                        Nachokumbuka cha mwisho ,Krisi alinisogelea karibu akashika shingo yangu akanisogeza karibu yake akanipiga busu ya kwenye paji la uso na busu la pili kwenye shavu langu la kulia.Aliniaga,kwa unyonge sana akachukua begi lake nililokuwa nalo mimi.Akanitazama sana na mimi nikiwa namtazama sana huku machozi yakiwa yamenilenga,nilimuaga kwa ishara ,akaanza kuondoka na mimi nikarejea shuleni kumalizia vipindi.
            Nilirejea shuleni nikiwa na furaha yenye mchanganyiko wa huzuni.Moyoni nikijiuliza ni lini nitakutana na wewe tena? Ni lini tutakuwa wote pamoja?
            Nilifika shuleni ,nikamalizia vipindi vilivyokuwa vimesalia. Siku zote siku ya ijumaa huwa ni fupi kwa ajiri ya waisilamu kwenda kuabudu.kwa hiyo ikifika saa sita vipindi vyote husitishwa,mpaka juma tatu.Wengine huenda kwenye vipindi vya dini na wengine huondoka kwenda nyumbani.
            Mimi niliamua kutoenda kwenye kipindi cha dini badala yake nilienda nyumbani.
            Sikumkuta mtu nyumbani ,mama alikuwa bado yuko kazini,Nikafika nikafungua mlango nikaenda kitandani kwangu,nikafika nikajilaza.
Muda kidogo  mama naye akafika kutoka kazini kwake ,nikaenda kumsalimia na kumpokea mzigo aaliokuwa amebeba mkononi .
Mama alianza kuandaa chakula cha mchana,nikasaidizana naye,hadi tukaivisha.                           
             Pendo ,mdogo wangu akawa amesharudi toka shuleni,mama akamwagiza alete maji ya kunawa na ya kunywa ,akatenga tukala chakula .Nilikula kidogo tu kwasababu bado nilikuwa nimeshiba chapati za kina Juma,nilinawa nikaenda kulala.
            Maisha yaliendelea ,usiku ule Krisi alimpigia simu Juma akamwambia kuwa amefika salama na anisalimie na kunipa taarifa hiyo.
            Safari ya maisha iliendelea nikiwa mbali na Krisi.Nilikuwa nasalimiana naye kwa muda mrefu nilipotaka kusalimiana naye kwa njia ya simu za watu mbalimbali kwa kuwa mimi nilikuwa bado sijanunua simu.
            Muda wa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ulifika nikafanya mtihani,nikamaliza.
            Baada ya kumaliza mtihani, niliingia mtaani na maisha mapya ya kitaa yalianza.
Bahati nzuri baba alininunulia simu baada ya kumaliza  mtihani, kwahiyo hii ilinirahisishia kuwasiliana na Krisi muda wowote niliohitaji kuwasiliana naye ,hata yeye kusalimiana na mimi kwa muda aliohitaji kuwasiliana na mimi.
            Baadaye nilipata safari ya kwenda Dare salaamu kumsalimia mama yangu mdogo.Aliniomba niende kwake kwa kuwa nilikuwa nimemaliza shule.
            Niliwasiliana na Krisi ili tukutane naye Nyegezi aniage.Kikwazo kilichokuja ni kwamba baba ndiye aliyekuwa ananisindikiza,nikamwambia aje kigogo jioni nilipokuwa kwa baba mdogo ili kusubiria kwenda nyegezi kesho asubuhi.
            Jioni ilipofika Krisi akiwa njiani kutoka Igoma kuja mjini, baba aliniambia twende  Nyegezi tukakate tiketi, nikajaribu kumkatalia nikamwambia ninataka kwenda kwa rafiki yangu perepetua ameniambia yuko Bugalika.Baba akaniambia tukitoka huko nitakuja niende.Nikawa sina jinsi ikabidi niondoke na baba mpaka Nyegezi.
            Tumefika stendi, tulikata tiketi,huku Krisi akawa ameshafika muda mrefu mjini akinisumbua kwa meseji kuwa kwanini sitokei?Nilimwambia kuwa baba amenibana sina chansi ya kuja huko sasa,nikamwomba anisamehe kwa usumbufu.
Akaniambia anarudi nyumbani,mimi nikamruhusu kwasababu baba hakutaka niende kuzurura zurura mjini  ndiyo maana alikuwa ananga’ana twende naye pamoja Nyegezi.
            Tulirejea nyumbani baada ya kumaliza kukata tiketi na jioni jioni ya saa moja tulienda milongo kwenye soko la joni ili nikanunue nguo nitakazoenda nazo huko.
            Tulipokuwa tumenunua kila tulichokuwa tunakihitaji tulienda nyumbani kupumzika .
Kesho saa kumi na nusu baba aliniamsha ili nijiandae tuwahi usafiri Nyegezi stendi.Nilienda kuoga,baada ya kuoga nilivaa nguo tayari kwa kuanza safari.
            Tulienda mpaka kwnye kituo cha daradara,na kwa muda mfupi gari ilipita tukapanda lkuelekea Nyegezi.
            Tulifika nyegezi kwenye saa kumi na moja na nusu asubuhi,tukafika tukapanda kwenye gari ya,,,,,,.
Baba aliniaga akaondoka kurudi nyumbani,na sisi safari ilianza ilipofika saa kumi na mbili tukaondoka Nyegezi kuiendea Dar.Nikiwa njiani baba alikuwa akinipiogia simu kuniuliza nilipokuwa nimefika.Krisi naye vivo hivo karibu safari yote niliongea naye akaniomba nisifike huko nikamwacha yeye na kuandamana na mwanaume mwingine.
Safari yetu haikuwa na matatizo yoyote hivyo kwenye mida ya saa tatu  saa nne tulifika  Ubungo.
Nilimkuta mama mdogo yupo stendi amenisubiria,akanipokea yeye na mtoto wake wa kike anaitwa Jenifa alikuja naye kuja kunipokea.
Baada ya hapo tulipanda gari za kwenda msasani,kwasababu yeye alikuwa anaishi Kinondoni shamba.
Tulishukia kwenye kituo kinachoitwa manyanya, tukaenda nyumbani anapokaa shangazi.
Usiku Krisi alinipigia simu kuniulizia kama nimefika salama,nikamweleza kuwa tulikuwa tumefika salama na sasa niko nyumbani.
Kesho yake ,nilichelewa kuamka sana,nilijikuta naamuka  saa tatu kwasababu ya uchovu wa safari.Niliamshwa kwa ajiri ya kunywa chai.
Nilinawa uso na kwenda kuoga,baada ya kuoga nilienda mezani kunywa chai.
Niipomaliza kunywa chai,Jenifa alinichukua tukaenda Kariakoo kutembea kwa kuwa ni sehemu niliyokuwa natamani niifahamu  kutokana na namna ilivyokuwwa inasifika sana huko nyumbani.Tuliondoka mpaka Kariakoo,tukatembea tembea.Nilipomaliza pale nilitamani pia nifahamu machinga complex ilipo.Basi Jenifer alinichukua tukaenda hadi Karume,nikakutana na soko la karume,nikataani kununua viatu.
Tuliingia mle tukaanza kutafuta viatu,lakini katika kutafuta aina ya kiatu niliyokuwa nahitaji nilijikuta simuoni jenifer,niliangaza pande zote nne za dunia lakini sikumwona.
Nikaanza kumtafuta ,nikajikuta nimepotea zaidi kwasababu ya ugeni wa soko  hilo.Hata njia ya kutokea nikawa siioni,nilizunguka sana kama nusu saa bila kuona mlango wa kutokea,nikafanikiwa kutokea kwenye stendi ile yya Karume sokoni.
Niliogopa kuulizia kwa hofu ya kuibiwa.Nikiwa natafakari jinsi gani nitaweza kurejea nyumbani,nikijiamini kuwa nitafanikiwa kutokana na kwamba nilifahamu ninakoelekea,ningemuuliza trafik akanielekeza,nilimwona Jenifer akiwa anaan gaza angaza huku na kule.
Nilimuita,aliponiona alifurahi sana,kwani alijiuliza ataenda kujibu nini nyumbani kwa kunipoteza.Tulifurahi,akanionyesha yale majengo ya machinga complex tukarejea nyumbani.
Siku nyingine tulienda cocobeach siku ya sikukuu ya Krismas.Tulipokuwa njiani tukienda msasani kupanda gari,kuna watu walituzunguka wakaninyang’anya simu yangu na kuchukua pochi ya dada Jenifa.Walitutishia kuwa tukipiga makelele wangetudhuru hata kutuua.Waliendelea na mchezo wao huo mchafu hasa kwa wasichana na baadhi ya wanaume na hakuna aliyeweza kuwazuia.tulilia tu na dada Jenifa kwa kupoteza vitu vyetu vya muhimu.
Ikatulazimu kutembea kwa miguu toka kokobeach hadi kinondoni shamba.Tulipitia barabara ya hail selase.
Huu ndio ukawa mwanzo wa kupoteza ,mawasiliano na Krisi.
 Nikiwa nasubiria matokeo, mama mdogo alinipeleka chuo kikuu huria kusomea kozi fupi ya mwezi mmoja ya kompyuta.
Matokeo ya klidato cha nne yalitoka ,sikufanya vizuri.Nilipata daraja la nne ya ishirini na saba.Wazazi wakata kunipeleka vyuo vya ualimu lakini mimi sikukubali kwa kuwa nilipenda sana kusomea utangazaji .Pia nilikuwa na hamu ya kusoma Advance.
Ikanididi nirejee nyumbani nikafanye tena upya mtihani wa kidato cha nne nipate sifa za kujiuunga na kidato cha tano na hatimaye chuo kikuu.
Nilipofika Mwanza,Nilianza harakati za kumtafuta Krisi mjini mwanza kuona huenda ninaweza nikagongana  naye.Nilikuwa kama kichaa,kwani nilitembea pasipo kuwa na mwelekeo,nilienda Kamanga,kuona huenda ninaweza kumwona pale kivukoni akivuka,sikumwona na nusura nigongwe na gari pale kamanga kwasababu nilitembea tu bila kuangalia kulia na kushoto.
Nilipomkosa pale nilienda  posta kwani kule kulikuwa na wanafunzi wengi waliokuwa wanaangalia matokeo ya kidato cha nne kwa kuwa kulikuwa na internet kefu kubwa.Sikumpata,nikarejea nyumbani kwa baba mdogo Igogo.
Kesho yake tena nikasafiri mpaka Igoma kuona kama ninaweza kubahatisha kumwona lakini hata hivyo sikufanikiwa.Nilijaribu kuuliza watu mablimabli lakini Krisi ninayemtaka mimi sikumpata.Nikarejea maskani.Siku moja nikiwa natembea tembea mjini nilikutana na rafiki yake Juma,nikamuuliza kama alikuwa na namba za simu za Juma,anipe,alinisomea,nikazisevu kwenye simu yangu.Niliamni nikimpata Juma nitakuwa nimempata Krisi.
Nilianza kumtafuta Juma kupitia namba ya simu niliyopewa na rafiki yake lakini hakuwa hewani.Nilijaribu kwa siku kadhaa bila mafanikio ,nikahisi huenda amepoteza simu au amebadili laini.
Niliposhindwa kumpata kwa njia hizo niligeukia mitandao ya kijamii,nikaenda kumtafuta  kwenye facebuku.kwa siku ya kwanza nilijaribu kumwangalia kwa majina ya Krisi,kama Kristofa,Christian na Krispirin hata hivyo sikumpta.Nikakata tamaa kuwa huenda hayuko kwenye fecebuku au amejiisajiri  majina mengine.
            Siku nyingine nikiwa na chati na marafiki zangu,niliiona sura ya Krisi akiwa ameandika statas lakini hakuwa anaiitwa Krisi,aliitwa Zakaria.Nilipofuatilia habari zake nikajilizisha ndiye yule Krisi wangu.
Nikamwomba urafiki(friend request),nikamwandikia na meseji ya kumweleza kuwa mimi ni aneth, nikampa na namba yangu mpya ya simu.
Nilienda kuangalia kama atakuwa ameitikia, hata hivyo hakuwa amefanya hivyo.Niliendelea na masomo katika shule ya sekondari ya Mwanza ,nikafanya tena mtihani,nikafanikiwa kufaulu.
Nikachaguliwa kujiunga na Nganza sekondari,nikasoma miaka yangu miwili pale hadi mwisho, nikafanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Sauti Mwanza.
Katika muda wote huo nilijitahidi kumtafuta Krisi bila mafanikio yoyote.Wanaume wengi walijitokeza kuhitaji mahusiano ya kimapenzi na mimi na wengine kuhitaji kunioa nikakataa.Niliamini kuwa ipo siku ningeonana na Krisi na kutimiza ahadi yetu ya kuishi kama me na mke.
Marafiki zangu walinikatisha tamaa mara kwa mara,kuwa nisihangaike na mtu ambaye hata hajulikani yuko wapi,na pengine kashampata mtu mwingine.Walinilaumu pia kuwakataa wanaume waliojitokeza kutaka kunioa kwa kuniambia mithali nyingi kama nafasi haiji mara mbili,ukiichezea utakuja kujuta.Lakini mimi  niliendelea kukaza kuwa nitamtafuta Krisi mpaka nimpate.
Mara kwa mara aliniijia ndotoni  na akilini mwangu kana kwamba yuko karibu.Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilipozidi kumpenda zaidi,ingawa simwoni.
Hata hivyo muda ulivyokuwa ukizidi kusonga nilianza kukata tamaa na ukiunganisha na maneno ya marafiki zangu yalinivunja moyo,nikamruhu mwanaume mmoja kuwa naye kimapenzi.
Tumeenda naye kwa muda wa mwaka mmoja na nusu,tukaanza kufanya mipango ya kuona.
Moyo wangu mara nyingi ulisita kwenda naye nyumbani kwao ili akanitambulishe,nikawa naahirisha safari kadhaa tulizopanga niende kwao akanitambulishe.
Alienda kuongea na marafiki zangu,wanishawishi nikubali kwenda wao.
Wakaja kuongea na mimi kwa kunirazimisha sana na kuniambia simulizi nyingi nikakubali,nikaenda kwao kunitambulisha.Nilikutana na wazazi wake wote.Ikabaki safri ya yeye kuja kwetu kuleta barua ya uchumba.
Siku zilivyokuwa zinaenda ,moyo wangu ulianza kupotea kwa Krisi,na kuhamia kwa Kelvin,mchumba wangu.
Mawazo yangu kwa Krisi yalizidi kutoweka baada ya Kelvin kuja nyumbani kwetu kuleta barua ya uchumba.Kelvin alijitahidi sana kuniondoa kwa Krisi kwa kunifanyia mambo mengi kama kunipeleka bichi ,shopingi na kwenye starehe mbalimbali.Kusema ukweli Kelvin alikuwa amenipenda kwa dhati,alifanya hivyo kwani marafiki zangu walimpa mkanda mzima wa kuhusu Krisi .
Wazazi wangu waliniiita nyumbani ili kwenda kukiri kama kwao kuwa kweli nimempenda na ninakubali kujifunga naye ndoa ,isije baadaye ikaleta shida.
Nikatoka chuoni, nikaenda nyumbani ambako nikama mwendo wa saa moja na nusu.Nikiwa katika Plantoni ya kutoka Mwanza mjini kwenda Kamanga ,niliona namba mpya ikinipigia,nilipokea nikatambua kuwa ilikuwa ni sauti ya mwanaume,akajitambulisha kuwa alikuwa Krisi.
Kwanza sikumwelewa vizuri kwasababu ya mawimbi ya ziwani ,baada ya kuvuka nikambipu,akapiga akajieleza sana kuwa ni Krisi yupi nikatambua kuwa alikuwa ni Krisi niliyekuwa ninamtafuta sana.
Leo hii amepatikana nikiwa nimempata mwingine ambaye tayari amejitambulisha nyumbani kwetu itakuwaje?
Nilifika nyumbani,nikawakuta wazazi wangu wote wapo ,lakini pia alikuwepo bibi na shangazi yangu.
Krisi alinipigia tena simu ,Nilimhoji sana kwanini hakujitokeza zamani zile nilipokuwa nikimtafuta akadai naye pia alikuwa akinitafuta na isitoshe alienda kusoma Uganda kwahiyo mwanzo alikuwa anapatikana mida ya likizo tu.
Alinieleza kuwa alikuwa anajaribu kunitafuta ingawa hakufanikiwa naya kwamba hana mchumba wala hajaoa.Namba yangu alipewa na Juma ambaye Juma aliipata kwa rafiki yangu mwingine niliyekuwa nakaa naye mtaa mmoja ila yeye alikuwa Morogoro walpokutana na Juma.
Nilimweleza ukweli kuwa mimi nina mchumba tayari na ameshajitambulisha nyumbani.
Alinisihi sana kwa kunikumbusha jinsi tulivyoahidiana kuwa tutapendana mpaka Mungu atakapotutenganisha,hivyo nibadili mpango wangu wa kuolewa na jamaa huyo.Nikiwa ninaendelea kuongea na Krisi mama aliniita kwenda kula chakula ili tuendelee na ratiba nyingine ya Kikao.
Nilienda kula,baadaye nikaekiti kuwa nimeanza kuumwa na tumbo ili kikao kisifanyike,baba kwa vile alivyokuwa ananipenda akawashauri wenzake kuwa kikao kifanyike kesho asubuhi.
Niliwaza sana jinsi nitakavyoweza kulitatua jambo hili,Krisi ndiye alikuwa yuko ndani ya moyo wangu lakini Kelvin alikuwa ananipenda sana,amenifanyia mambo mengi,nikimwambia nimeahirisha anaweza hata akajidhuru au huenda kunidhuru,nitawaambiaje wazazi wangu ambao wamekuwa wakiletewa zawadi nyingi na Kelvin,nilizozileta mimi mwenyewe?
Usiku kucha niliwaza mambo hayo pasipo kupata majibu.kulipokucha nilipata wazo kuwa nimuite shangazi nimweleze ukweli ili yeye anisaidie kuwaambia wazazi .
Nilimuita shangazi nikamweleze picha yote jinsi ilivyo.Hata yeye hakuwa na majibu,alitikisa kichwa tu na kuniuliza swali ,tutafanyaje sasa mwanangu?
Lakini akaniahidi kwenda kuongea na wazazi wangu waone jinsi watakavyolitatua swala hilo.
Walipomaliza kunywa chai.Saa tatu shangazi aliwaita wote kuwa kuna jambo gumu wanalotakiwa kulijadili kabla hawajaongea na mimi.
Walikaa kikao,shangazi akawafungulia mkanda wote.Mama alichukia sana,kama ada yake  kwani yeye ndiye alikuwa mkali zaidi hata ya baba,akaniita ,lakini baba akamkataza kuwa wajadili kwanza hoja iliyo mezani,wataniita.
Walijadiliana na  mwisho wa kikao hicho wakaniita,wakasema kuwa wamekubaliana kusitisha suala la uchumba wangu,na ili kumsaidia mwenzangu(Kelvin) ninatakiwa kumdanganya kuwa kunamatatizo Fulani yamejitokeza wamekubaliana hadi mwakani,baadaye nianze kuwa mbali naye kidogo kidogo mpaka atakapoona mwenyewe kuwa sitaki kufunga naye ndoa.
Nilirejea chuoni,Kelvin alinipokea akitaka kujua sababu ya wazazi kuniita nyumbani.Nilimwambia kama wazazi walivyonieleza kuwa wameona maswala haya wayahamishe mwakani kwahiyo awe mvumilivu.
Kelvin alihoji sana kwanini wameamua hivyo wakati mimi kila kitu kiko sawa ,uwezo wa kuandaa harusi ninao?
Nikamwomba awe mvumilivu,nikijua kuwa ukweli kuwa ,huo ndio ulikuwa mwisho wake.
            Tuliendelea kuwasiliana na Krisi alikuwa anafanya kazi Tanga katika kiwanda cha simenti,akaniahidi kukutana naye wakati wa likizo yake.
Huku nako nilijitahidi kumukwepa Kelvin aliyetaka kila sehemu twende naye,kwa visingizio vya ugonjwa ,uchovu na ushauri wa kutunza pesa kwa ajiri ya maisha ya baadaye.
Tabia hii ilipokuwa endelevu aliwauliza marafiki zangu,wakamwambia ukweli kuwa tayari nilikuwa nimeshapata Krisi.
Aliniarika kwenye chakula cha mchana,nikaenda.Akaniambia kuwa tayari alikuwa ameshajua kwanini nimekuwa sitaki kwenda naye kama ambavyo amekuwa akiniomba,na mimi nikamweleza ukweli tu.Alijitahidi kunibembeleza nibadili maamuzi yangu,nikumbuke kuwa tayari alishanipeleka kwa wazazi wake atawaambia nini? Na alikuwa ananipenda sana.Aliongea kwa hisia kubwa,kiasi cha kwamba macho yalinilenga ,nikamuhurumia sana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kama nilivyokuwa nimeamua.Si kosa langu mimi kwenda kwao ,yeye ndiye aliyenilazimisha, mimi nilikuwa sitaki.
Nilipoendelea na msimamo wangu alinipa muda wa kwenda kufikiria zaidi.
Niliendelea kuongea na Krisi akaniahidi kuwa akija atafanya mipango ya kufunga ndoa.Hii ikafanya  mawazo yangu kwa Kelvin kutokomea katika vyumba vya moyo wangu.
Kelvin alimaliza chuo ,yeye alikuwa amenitangulia mwaka mmoja akaenda kwao,Shinyanga.Aliondoka bila hata kuniaga,kwa kuwa nilikuwa kama nimemsariti.Mimi niliendelea na chuo,nikamaliza.
Krisi alikuja Mwanza,nikampokea katika stendi ya Nyegezi,tukaenda kwao akanitambulisha.Baadaye tulifunga ndoa tukawa mme na mke.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni