“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu
aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na
kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke
wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa
tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake
yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna
ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi
nimwam
bie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa
utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu
badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa
nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya
akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si
mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi
kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu
kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye
ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa
jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali
kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary.
Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote
yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke
wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya
kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba
yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na
atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia
talaka ile na kuichana vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10
alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea
huruma kwa muda, rasilimali na nguvu
alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa
sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa.
Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele
yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia.
Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.
Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua
kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea
kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.
Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa
sana nikakuta mke wangu akiandika jambo
mezani. Sikutamani hata kula chakula
alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani
na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu
nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa
mtu na Mary
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa
bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema
shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi
masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote
kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi
mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba
kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja
sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya
upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana.
Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu:
mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya
mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo
hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa
sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo
kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa
na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi
nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya
harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba
katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe
nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango
wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia
kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho
zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti
yake ya ajabu.
Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana
na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni
ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani
talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau.
Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu
nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo
nilipombeba kwa mara ya kwanza sote
tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga
makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama
mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma
moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu
hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni
zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu.
Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya
upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka.
Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya.
Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami
nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya
pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea
kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi
aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua
kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu
kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti
tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake
zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo
wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini
namfanyia hivi.
Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati
yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi
nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya
tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi
yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary
kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia
kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi
likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila
siku kuliniimarisha zaidi.
Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi.
Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa.
Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa
kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu
amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza
kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma...
mke wangu ana uchungu na maumivu makuu
moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa
kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na
kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama
muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba
mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu
alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na
akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso
wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya
mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu
kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka
mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka
shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili
wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu.
Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.
Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata
kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda
shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia
sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo.
Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata
bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu
ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi.
Mary alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani,
Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.
Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa
kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa
mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary,
nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani
ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu
sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke
wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo
tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa
kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda
mke wangu sitamuacha mpaka kifo
kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba
kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na
kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka
zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza
maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu.
Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi.
Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila
asubuhi mke wangu mpaka kifo
kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani
na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa
usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa
na maiti ya mke wangu kitandani.
Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na
saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa
kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa
Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka
asiniingize katika chuki na mwanetu kama
ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni
mume mwema….................
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni