Kuna vijana walikuwa wamekaa kijiweni
huku wakizungumza, ghafla akapita kijana mmoja anaitwa Sudi na
aliwasalimia, huku akiwa anaendelea na safari yake kwa bahati mbaya
aliteleza na kuanguka, lakini hakuna hata kijana mmoja aliyenyanyuka na
kumsaidia wote waliangua vicheko na mmoja wao akisema "Huyu jamaa
atakufa kwa mawazo, si anaishi hapo mtaa wa pili kwa ndugu zake yaani
hawana chochote ni masikini sana kazi yao ni kuombaomba" Huku
wakiendelea kumcheka.
Sudi alinyanyuka na kuendelea na safari
bila ya kuzungumza chochote huku machozi yakionekana kumlengalenga
aliwaza moyoni mwake "Watu wengi wananidharau kutokana na hali duni ya
maisha niliyonayo, eeh Mungu nisaidie" Pale kijiweni waliendelea
kuzungumza "Unajua umasikini ni mbaya sana, kwani siku zote ukiwa
masikini, basi ujue utapata shida sana, na ukizingatia yule aliyenacho
ndiyo anazidi kuwa nacho."
Mmoja kati ya wale vijana alikuwa anaitwa Frank alisimama na kusema "Hivi mbona mnadharau sana jamani, unajua usimdharau mtu usiyemjua kumbukeni kuna leo na kesho, na hakuna binadamu anayependa kuishi maisha ya shida, msikufuru jamani mshukuruni Mungu kwa kuwa nyinyi mna maisha mazuri, familia zenu ni matajiri lakini kumbukeni msitumie pesa kama fimbo ya kumchapia yule asiyenacho".
Mmoja kati ya wale vijana alikuwa anaitwa Frank alisimama na kusema "Hivi mbona mnadharau sana jamani, unajua usimdharau mtu usiyemjua kumbukeni kuna leo na kesho, na hakuna binadamu anayependa kuishi maisha ya shida, msikufuru jamani mshukuruni Mungu kwa kuwa nyinyi mna maisha mazuri, familia zenu ni matajiri lakini kumbukeni msitumie pesa kama fimbo ya kumchapia yule asiyenacho".
Wote walimcheka na kusema "Kwenda zako,
sisi watoto wakishua wewe, hatuwezi kujichanganya na marafiki kapuku
kama wewe" Basi Frank aliondoka huku akisikitika sana. Baada ya kama
wiki moja pale mtaani kulitokea ugomvi baadhi ya wale vijana walihusika
kumpiga sana kijana mmoja anaitwa Juma wa pale mtaani ndipo
walipokamatwa vijana wengi katika mtaa ule na kupelekwa mahabusu,
katika wale vijana na Sudi alikamatwa ijapokuwa hakuhusika, Baadaye
Askari walitoa adhabu kwa vijana wote kufanya kazi ya kungoa kisiki kila
mmoja alipewa sehemu yake, na walikuwa vijana kama saba. Kila mmoja
alikabidhiwa sehemu yake na walipewa muda wa siku tatu tu wawe
wamekwisha maliza.
Sudi alifanya ile kazi kwa juhudi zote
ili afanikiwe kurudi nyumbani na hatimaye kutokana na juhudi ndani ya
siku moja tu alimaliza. wale wengine walishindwa hata kufikia nusu
kutokana na kuwa ni wavivu na walikuwa hawawezi kazi ngumu, kwa moyo wa
huruma Sudi alijitahidi kuwasaidia wenzake kwa kila hali bila ya kujali
kuwa walikuwa wakimdharau na kumuona hafai lakini alimsaidia kila mmoja
na baada ya siku tatu waliachiwa huru.Kutokana na kilichotokea wale
vijana walimshukuru sana Sudi, na kumuomba samahani. Sudi aliwasamehe
bila ya kuweka kinyongo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni