Monalisa alinyanyuka na kufungua mlango
kumbe alikuwa amekuja wifi yake ambaye alikuwa ambeba begi lake kubwa
na mfuko wa Rambo, Alimkaribisha ndani na kumsaidia kubeba begi. Wifi
huyu alikuwa ametokea Kijijini Morogoro na alifika kwa kaka yake ili
aweze kutafutiwa shule, Basi alikaribishwa vizuri bila matatizo yoyote,
Kutokana na nyumba kuwa ndogo ilimbidi ajumuike kulala pamoja na watoto
pale sebuleni ambapo walikuwa wakitandika godoro na kulala pamoja.
Maisha yaliendelea, huku wifi akiwa anaishi pale nyumbani, siku zote
alikuwa akiamka asubuhi lakini asimsaidie Monalisa kufanya kazi yoyote.
Hivyo Monalisa alikuwa akimka mapema
nakuandaa kifungua kinywa na wakati mwingine ilimbidi apike chakula
asubuhi kwaajili ya kuwaachia watoto halafu ndiyo aondoke kwenda kwenye
biashara yake ya kuuza samaki.Maisha yaliendelea hivyo hivyo ndipo
sikumoja Monalisa aliamua kumueleza mume wake tabia za mdogo wake kukaa
bila ya kufanya kazi yoyote na ukizingatia alikuwa ni msichana mkubwa,
Jerome alijaribu kumwelekeza mdogo wake bila mafanikio kwani sasa ndiyo
alileta mtafaruku zaidi kati ya Monalisa na wifi yake, sasa Wifi alianza
kununa bila sababu na kumchukia sana wifi yake.
Hali ile ilikuwa inamuumiza sana
Monalisa ambaye alikuwa akihangaika siku zote ili nyumbani watoto waweze
kupata chakula, na Mume wake alikuwa ni fundi seremala, na hata
alipokuwa akipata pesa mara zote alikuwa akimpa mdogo wake kwahiyo
ilimbidi Monalisa, ajibane sana katika kutafuta pesa kwaajili ya
matumizi ya pale nyumbani. Baada ya miezi sita kupita wifi yake Monalisa
vituko ndiyo vilizidi sasa alianza kuleta wanaume pale nyumbani. Siku
zote alikuwa akisubiri watoto wakiwa wameenda shule, na Baba na Mama
wakiwa wameenda kazini, na kutumia muda huo kuingiza wanaume, na huku
akitumia kitanda cha kaka yake bila ya kujali chochote, tabia hiyo
iliendelea hadi siku ambay
o Monalisa aligundua kuwa shuka lilikuwa limechafuka na kumuuliza wifi yake ambaye alikasirika sana.
o Monalisa aligundua kuwa shuka lilikuwa limechafuka na kumuuliza wifi yake ambaye alikasirika sana.
Huku akiwasingizia watoto walikuwa
wakicheza kitandani, lakini watoto walikanusha huku wakilia kuwa
wamesingiziwa. Baadaye Monalisa alipuuzia lakini wifi yake hakuacha hiyo
tabia, ndipo siku moja jirani aliamua kumueleza Monalisa kile
kinachoendelea akiwa hayupo.Monalisa alisikitika sana na sasa aliwaza
namna ya kumfumania wifi yake.
Siku hiyo alikwenda kazini kama kawaida
lakini hakukaa muda mrefu akawa anawasiliana na yule jirani ambaye
alimwambia kuwa muda huo kuna mwanaume amefika pale nyumbani. Moja kwa
moja Monalisa aliondoka kijiweni na kurudi nyumbani ambapo alimkuta wifi
yake akiwa amejipumzisha kitandani kwake na mwanaume huku wakifanya
starehe zao, Alishtuka sana na kuanza kumfokea huku akimtaka
aondoke."Wifi nimekuchoka, naomba uondoke, aibu gani hii jamani,
unawafundisha nini watoto wangu naomba uondoke sitaki kukuona kabisa"
Wifi kwa hofu alianza kulia na kuomba
msamaha kwa Monalisa asimueleze kaka yake.Lakini Monalisa alimuambia
haiwezekani amekwisha mvumilia vya kutosha lazima aondoke, Baadaye
Jerome aliporudi kutoka kazini Monalisa alimweleza kila kitu ndipo kaka
mtu alipoamua kumrudisha mdogo wake kijijini kwa kuchoshwa na tabia za
mdogo wake.Wifi aliomba msamaha, na Monalisa alimsamehe lakini
alimwambia ni vyema angerudi nyumbani Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni