Jumatatu, 6 Julai 2015

MOYO WA KUPENDA

AJALI mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya sabasaba nje kidogo ya mji wa Musoma iliwashangaza watu sio tu kwa jinsi ilivyokuwa ajali ya mbaya sana lakini kwa namna gani wahusika waliweza kutoka wakiwa bado wanavuta pumzi.
Hayakuwa makosa ya dereva bali makosa ya wakandarasi waliokuwa wakitengeneza daraja. Hawakuweka alama zinazoonekana vyema kwa madereva juu ya ukarabati uliokuwa ukiendelea mbele.
Bwana Johnson pasi na kujua akiwa na mkewe ndani ya gari mwendo wa kawaida tu wa kilomita 65 kwa saa walifikia eneo lile wakitambua wazi kuwa mbele palikuwa na njia.
La haula! Palikuwa na shimo kubwa sana na refu kuelekea chini!!
Gari ikaenda hewani.

Jinsi Mke Wangu Alivyo Aga Dunia

Niliingia nyumbani nikamkuta mke wangu akiniandalia chakula cha usiku. Nilimshika mkono na kumwambia: “Nina jambo ninalotaka kukueleza.” Alikaa na kunisikiliza kwa makini. Dalili za wasiwasi nilikuwa nikizishuhudia machoni mwake.

Ghafla nilijikuta katika hali ya kushindwa kukifungua kinywa changu. Lakini ilikuwa ni lazima ajue ninachokifikiria, hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa upole: “Ninataka tuachane.” Hakuonekana kuudhika kwa hoja niliyokuwa nimeiwasilisha mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa: “Kwa nini?”

Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo alighadhibika sana na kuniambia kwa sauti ya juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule hatukusemeshana, na muda wote alikuwa akilia. Nilitambua kuwa alitaka kujua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu lenye kuridhisha; kwa sababu sikuwa na mapenzi naye tena, moyo wangu ulikuwa umetekwa na binti mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!

Huku nikiwa na hisia za hatia moyoni mwangu, niliandika pendekezo la talaka ambalo lilieleza kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya asilimia 30 ya kampuni yangu. Aliitazama karatasi hiyo kisha akaichana na kuitupa kwenye ndoo ya takataka. Mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa muda wa miaka kumi alikuwa amegeuka kuwa kama mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba radhi kwa kumpotezea muda, rasilimali na nguvu zake lakini sikuweza kutengua kauli yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli ndani ya huba lake na kuwa teja wa penzi lake. Hatimaye alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo nilikuwa nikitarajia kuliona. Kilio chake kwangu kilikuwa kama faraja. Wazo la talaka lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi kupata nguvu na sasa lilionekana kuwa wazi kabisa.

Jumatatu, 15 Juni 2015

NDOA YANGU INANITESA





Nilikuwa nikifanya kazi katika kampuni moja ya usafirishaji wa madini kutoka Tanzania kupeleka Bang kok nchini Thailand. Kampuni yetu ikiwa ya mtu binafsi na ilikuwa Mkoani Arusha. Mimi Sweedy Kachenje ndiye niliyekuwa idara ya usafirishaji, nikiwa afisa mauzo.
Katika maisha yangu yote nilitegemea sana na nilihitaji kuwa na mwenzi wa kuishi naye, kama vile familia

SAHIHI YA KIFO

SEHEMU YA KUMI NA TANO

“ I hate boys just leave me alone please, I hate
you
go,”( tafadhali naomba uniache mwenyewe
nawachukia wavulana, nakuchukia nenda)
dada huyo alizidi kumpigampiga david huku
akirudia maneno hayo kwa lugha ya kingereza
bila

SAHIHI YA KIFO

SEHEMU YA KUMI NA NNE

Maisha ya david yalianza kubadilika chuoni hapo
baada ya kumpata rafiki mmoja wa kiume
alieitwa
gozbety lakini yeye alikuwa anapenda kujiita
gozbety CT 234 ambaye ni mwenyeji wa hapo
hapo

SAHIHI YA KIFO

SEHEMU YA KUMI NA TATU

Kwakuwa afande criss alikuwa in mtu mzima pia
hakuvaa kipolisi alikwenda kama raia wa kawaida
hivyo yeye aliandika anakwenda kwa mkuu wa
gererza na divid aliangalia jina moja la juu baada
kama ya majina matano hivi akaliandika kuwa
anakwenda kumuona mtu yule kumbe hata kumjua
hamjui ila lengo lilikuwa in kutaka kuonana na
wafungwa angalau anaweza akapata chochote kitu
juu ya kifo cha baba yake..

SAHIHI YA KIFO

 SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Upande wa mama victoria ambaye alimuona david
kule saluni, alionekana kukosa amani tangu alipo
muona david,
alijikuta akifikiria mambo mengi sana hasa ukweli
na siri nzito alio nayo ndani ya moyo wake,
alitamani kuonana na familia ya kina david ili
awaelezee juu ya ukweli huo lakini hakupata nafasi
hiyo maana hakujua wapi wanapatikana,