Jumatatu, 15 Juni 2015

SAHIHI YA KIFO

 SEHEMU YA TISA

Hayo maneno yaliwatoka watu tofauti katika eneo
hilo na wakati huo wakina mzee nyomolage
walitumbukia ndani ya kaburi na kumtoa mzee
kazinge, taarifa ziliweza kuwafikia mapaparazi
ambao walitoka kwenye kwenye vituo tofauti

tofauti kama vile redio,magazeti na hata wale wa
televisheni ili kukusanya habari hiyo amabayo
walijua kuwa lazima itawapatia pesa ya kutosha
kutokana na uzito watukio hilo picha nyingi
zilipigwa ili kupendezesha magazeti..
Padri aliamrisha wazike maana mvua ilianza kuwa
kubwa watu walimfukia mama david kwa haraka ili
mvua ile iliyo kuwa inanyesha isije ikaleta balaa
lingine wakashindwa kuufukia mwili wa marehemu
magrety.
David alilia sana maana hakuamini kama mama
yake ndio safari yake imefika mwisho,
Wale askari walimshikilia mzee kazinge ambaye
alikuwa anavuja damu kwenye mguu ule ulio kuwa
umepigwa risasi, mama muksini nae hakuwaacha
watoto wake nisha na dasoni.
Upepo ulizidi na mvua ikawa kubwa na weusi ulio
sababishwa na mawingu ukawa umetawala kijijini
hapo na bahati nzuri zoezi la mazishi likawa
limeisha japo kwa shida watu walitawanyika
kuikimbia mvua ile, askari nao wakataka kuondoka
na mzee kazinge lakini mzee kazinge aliomba
azungumze na wanae hasa david ndipo alipoitwa
david baada ya mama muksini kuondoka na kina
nisha kwa kuwa wale ni watoto na hali ile ya hewa
ingeweza kuwaletea homa,
”David mwanangu hakika umeelewa binaadamu
walivyo naomba ujifunze kupitia matatizo haya
penda kuwa mtu wa kusikiliza na kuongea kidogo
tu ili uweze kuwajua wabaya wako, usiwe na
papala kutaka kupata mali zako fuatilia taratibu
iliuweze kukamilisha ushahidi utakao weza
kuwarudisha tena nyinyi katika maisha mazuri
ambayo mwanzo mimi nilikuwa naishi, sasa
nakuruhusu nenda mjini karudishe mali zako wewe
na wadogo zako nakukabidhi famulia hii uilee kadri
utakavyo weza ili wasije kupata machungu zaidi
pale watakapo tukumbuka sisi na ukifika huko
mtafute yule mama anayeitwa magdalena ambaye
aliniambua kuwa anaushaidi utakao weza
kurudisha mali zenu nakutakia kazi njema na
maisha mema uwezekano wangu wa kutoka
gerezani ni mdogo sana kwaheri mwanangu
wasalimie wanangu waambie nawapenda sana”
Alipo maliza tu kusema askari nao wakamkokota
mpaka kwenye gari lao kisha kuondoka nae david
hakuwa na cha kufanya zaid ya kuangalia tu lile
gari huku moyo wake ukiwa umesha badilika kuwa
wa simba kwa yeyote atakaye leta mchezo na
familia yake. Mvua ile kubwa iliyo kuwa
inamnyeshea ilikuwa in kama vipande vya barafu
ambavyo vina peperushwa na upepo hakujali
jambo ilo mpaka watu wazima walipo kwenda
kumtoa pale kwenye ile mvua kwa nguvu,
Akili ya david ilikuwa imesha changanyikiwa kwa
matukio ambayo yamemtokea mfululizo tena
yalikuwa chini ya umri wake lakini hakuwa na budi
kukubaliana nayo ili ajue wapi anaanzia, mpaka
pilika pilika zote zinaishia ilikuwa tayari
imeshatimia mishale ya saa kumi na mbili jioni,
hivyo kutpokana na ile mvua wengi walikwenda
majumbani kwao ila wale walio kuwa karibu na
familia ile ndio walio baki kwa kina david kuwa
fairiji kama vile mama coolin, mama muksini kina
mzee nyomolage na wengine,
Baada ya siku tatu swala la msiba likawa limeisha
kilicho baki ilikuwa in kujua kuwa wata wasaidia
vipi wale watoto hasa nisha na dasoni amabo
walikuwa wadogo maana david anakabiliwa na
majukumu mazito ya kutaka kurudisha haki ya
familia yake.
Mama muksini hakuchoka alijitolea kuwa chukua
na kuwalea lakini akasema kwa sasa mume wake
hayupo yupo safari kwa muda wa miezi sita sasa
maana anafanya kazi katika mbuga za wanyama
hivyo huchukua muda mrefu mpaka kurudi lakini
kwa sasa hana muda atakuwa amerudi baada ya
siku kama nne hivi mbele hivyo atazungumza nae
ili ajue na yeye atalipokea vipi na kama atalikubali
jambo hilo basi atakaa nao na kujitahidi kuwa
somesha mpaka pale mungu atakapo wasaidia
kupata kazi yao.
Wote walikubaliana juu jambo hilo david alikuwa
hana chakusema zaid ya kuwasikiliza tu japo
kichwani mwake alikuwa anaonekana kufikiria
jambo fulani ambalo hakutaka kuliweka wazi kwa
wakati huo mbele ya hadhara ile ya watu wake
wakaribu,
Sikuzilikatika na bwana wa mama muksini akawa
karejea kutoka ile safari yake aliyo kuwa
amekwenda alipo fika tu nyumbani kwake
aliwakuta kina nisha na dasoni wana jilia chakula
cha mchana jinsi alivyo kuwa na roho mbaya baba
ya huyu japo alizipata taarifa za msiba na
matatizo waliyo yapata watoto hao alidiliki
kumuita mke wake na kumuuliza swali mbeye ya
watoto hao mke wangu kituo hiki cha kulelea
watoto yatima kimesajiliwa lini maskini wa mungu
nisha alipaliwa na chai kusikia maneno yale ya
kejeli
“mume wangu maneno gani hayo unazungumza
mbele ya hawa watoto ndio kwanza umetoka
safari si ungepumzika kwanza kisha tuyazangumze
vizuri’?mama muksini alimwambia mumewe
Ghafla mama muksini kalamba kibao cha uso aja
kaa sawa kasukumwa aelekee chumbani, nisha
kuona vile akanyanyuka na kumshika mkono
dasoni wakakimbia mama muksini alipo taka kuwa
fuata mumewe akamzuia na kumpa maneno ya
vitisho,,,
“kama utathubutu kutoa mguu wako hapa ndani
na kuwafuata wale watoto jua kwamba ndio
umevunja pingu tulio funga mimi na wewe,
nimekaa mimi na wewe miaka kibao hapa hata
kusema mume wangu leo nimejisikia kichefuchefu
hakuna halafu unataka kuniletea vipaka vyako
hapa ndani baradhuli mkubwa wewe”
Mama muksini matumaini yake ya kutaka kuwalea
kina nisha yaligeuka na kuwa fadhaa, kilio
kikamsindikiza mpaka chumbani na huko kukawa
hakuna neno walilo kuwa wanazungumza zaidi ya
mumewe kumsema tu kwa kujichukulia maamuzi
kama yeye ndie mtafutaji.
Nisha akawa anamkimbiza dasoni waelekee
nyumbani kwao lakini hakika mwenyezi mungu in
mkubwa na alipangalo yeye hakuna anayeweza
kulipangua na watu wanaweza kushilikisha
maamuzi yake na uchawi kama tatizo likielemea
kwenye famila moja wakati,
Walipo kuwa kwenye mwendo huo ambao
ulisababishwa na kitendo kilichofanywa na mume
wake mama muksini cha kuongea kauli za
kuwanyanyapa watoto wale na kumpiga mkewe
kwa sababu yao kiliwafanya kutokuwa makini
wakati wakikimbia maana machozi pia yalikuwa
yanawatoka kwa hasira punde si punde sauti
iliyokuwa inaomba msaada ilisikika,,,,
“mama nakufaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!! !!!!!”
Hapohapo na sauti za vioo vya gari lile kubwa lililo
kuwa limepakia viazi vilisikika vikivunjikavunjika,
watu wengi walionekana kukimbilia eneo lile
kutaka kujua nini kilichotekea huko.
“”ajali jamani ajali mungu wangu ni wakina nani
hawa” watu walikuwa wanazungumza
Baada ya watu kuwa wengi na kulizunguka gari lile
lililo ingia mtaloni na kuona maiti ya mtoto mmoja
wakiume baadhi ya watu walio kuwa wamemjua
mtoto huyo waliangua kilio papo hapo na kila
mmoja yalimtoka mengi mdomoni,,,,
“Kijiji hiki kina wachawi sana wamewakosea nini
familia hii ni juzi tu tumetoka kumzika mama yao
leo mtoto huyu naye ameaga dunia”
“Maskini dason ameaga dunia bila hatia”
“Nani ameaga dunia? Mtu mmoja aliuliza alihisi
kama amesikia vibaya vile,
“ ni dasoni mtoto wa mzee kazinge”
jamaa yule alivyosikia vile alitimua mbio kumfuata
david nyumbani kwao na alifika haraka sana
maana hapakuwa mbali sana na ajali ilipo kuwa
imetokea, alinzaa kugonga huku akihema,
“david david david!!!!
Kila alipo kuwa anaita akawa hajibiwi akaamua
kuchungulia dirishani hakuamini alicho kiona kitu
alicho kuwa anataka kukifanya david,,,,,
We david nakuomba usijiue rafiki yangu, nakuomba
sana sio kitu kizuri unachotaka kuki fanya kwa
wakati huu fikiria wadogo zako, kwanza mguu huu
nimekuja kwako kunatatizo limewapata wadogo
fanya haraka twende acha hicho unacho taka
kukifanya hakina faida nakuomba…
David aliachia kikombe kile kilichokuwa na maji
machache na kuzimwaga dawa zile zilizo kuwa
mchanganyiko kwa mshangao baada ya kusikia
wadogo zake wamepatwa na tatizo, alizubaa kwa
muda na kukurupuka kufungua mlango kisha
kutoka nje yule jamaa akampokea mlangoni na
kuanza kukimbia nae mpaka kwenye tukio lile
Alifika pale na kuukuta mwili wa mtoto mdogo
umefunikwa na kanga alipo ufunua alimkuta
dason,,
Maskini wa mungu david alilia kama mtoto mdogo
vile, makamasi yalishuka mpaka mdomoni mwake
ghafla akamkumbuka nisha,,
“Nisha wangu yuko wapi jamani”
“ nisha dada uko wapi njoo dada umejificha
wapi”??
david akawa anaita huku anazunguka kila upande
watu hawana la kufanya maana wengine wakujua
kama watoto hao wapo wawili ila baadhi ya watu
walio kuwa wana mjua wakawa wazunguka
kwenye majani kumsaidia kutafuta na wengine
wakajumuika pia,,,
“jamani kuna mtoto wa kike huku ila bado
anahema” mzee mmoja alifanikiwa kumuona nisha.
David ilimbidi aelekee kule alipofika alimkuta nisha
kaumia vibaya baada ya vioo vile kumchana
mgongoni na vingine kung’a ng’ania mwilini
mwake watu hawakua na muda wa kupoteza
wakamkimbiza nisha hospitali na kumuacha david
pale na maiti ya dasoni.
Tarifa ziliwafikia kina mama muksini na mumewe
hofu ikatanda kwao, mzee nyomolage naye
aliyekuwa shambani kwake aliweza kupata taarifa
hizo naye aliwahi kufika kwenye tukio ambapo
alikuta polisi wameshafika pale wakifanya taratibu
zao ambapo iligundulika kuwa na dereva wa gari
hilo naye amefariki dunia.
Hivyo polisi walitoa agizo kuwa wanandugu waka
zike maiti ya mtoto huyo dason maana ilikuwa
imeharibika vibaya na isingeweza kukaa
mudamrefu ingeaza kutoa harufu,
Hawakua na budi kufanya hivyo taratibu zote
zilifuatwa kaburi lilichimbwa pembeni ya mama
david na david kwa mara ya pili alibeba msalaba
wa mdogo wake.
Dasoni alifukiwa akawa amemfuata mama yake
mbele za haki yani ikawa pigo ndani ya pigo.
David alizidi kuisha kiafya kutokana na mambo
yalio kuwa yanamkabili na hakuwa na msaada wa
maana japo alishukuru kwa moyo waliouonesha
kina mzee nyomolage juu yake,
Usiku na mchana ulipokezana na siku zikasogea
nisha naye akawa ametolewa hospitali na kupewa
taarifa juu ya kifo cha dasoni kiukweli alilia kama
msiba ulikuwa unaanza upya vile.
Wazee walikaa kikao nakulijadili swala la msiba
ulivyo mfika dason hali ya kuwa alikabidhiwa
mama muksini. nisha ilimbidi kueleza kilichotokea,
na ndipo wanakijiji wakafikia muafaka kuwa
watamtenga mume wake na mama muksini.
Wakati kikao kilipo kuwa kinakaribia mwisho
alikuja afisa mmoja ambaye alijitambulisha na
kusema kuwa ametoka mahakama ya wilaya
akawapa barua kuwa mzee kazinge atafikishwa
mahakamani kesho hivyo wanaombwa familia yake
kufika huko
Wazee hao waliipokea barua na kuisoma na muda
uliwaonesha kuwa saa saa tatu asubuhi
wanahitajika kwenda kusikiliza hukumu ya alfredi
kazinge katika mahakama hiyo ya wilaya
****************
Adhana ya saa kumi na moja alfajiri iliyokuwa
inawakumbusha waislamu kwenda kufanya ibada
iliweza kumuamsha david toka usingizini na
kuegemea mto ulio kuwa kitandani na kuonekana
akitafakari jambo fulani hivi ambalo liliweza
kumyanyua pale kitandani na kuelekea chumbani
kwa wazazi wake.
Aliwasha mshumaa ili aweze kupata mwanga kisha
kufungua sanduku dogo ambalo lilikuwa
limewekwa chini ya uvungu wa kitanda na kutoa
baadhi ya makaratasi ambayo yalikuwa na picha
ndogo ya mzee kazinge kwa juu upande wa kulia.
Aliyangaalia kwa makini maelezo yale ambayo
yalikuwa yanaonesha uhitimu wa chuo kikuu cha
biashara ambacho alisoma mzee kazinge, kisha
akatoa albamu ya picha na kuanza kuzitazama
moja baada ya nyingine alitoa tabasamu kidogo
baada ya kuona picha ya baba yake kwa mavazi
ya kizamani aliyokuwa amevaa lakini hali hiyo
ilibadilika ghafla baada ya kuona picha aliyo piga
baba yake na marehemu mama yake siku ya ndoa
yao,
David hakusita kupeleka kiganja chake cha mkono
kwenye sura ya marehemu mama yake nakuanza
kukizungusha juu ya picha hiyo, alikumbuka
upendo wa marehemu mama yake tangu alivyo
kuwa hai mpaka umauti unamfika hivyo
aliinyakuwa picha hiyo mpaka kwenye mdomo
wake na kumpa busu la heshima mama yake na
baada yapo akatoa ishara ya msalaba
iliyomaanisha pumzika kwa amani.
Alizibeba baadhi ya picha kama kumbukumbu na
kuelekea chumbani kwa nisha, aliufungua mlango
taratibu bila kuingia ndani akawa anamwangalia
mdogo wake kipenzi aliye bakia, alihuzunika baada
ya kutupa macho kwenye kitanda cha pembeni
ambacho alikuwa analalia marehemu dason, david
alishindwa kuvumilia aliufunga ule mlango kisha
kuelekea chumbani kwake.na kuziweka zile picha
kwenye mkoba wake na kutoka nje kuandaa
kifungua kinywa cha asubuhi ili waweze kuelekea
mahakamani muda utakapo wadia.
ITAENDELEA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni