Jumatatu, 15 Juni 2015

SAHIHI YA KIFO


 SEHEMU YA PILI
Daktari alimtoa mikono David kisha kumshika
begani na kumueleza........
”hali ya mama yako inaridhisha kiasi ila kuna
mambo inabidi tukazungumzie ofisini kwangu”
Walifuatana mpaka ofisini na dokta alianza kumu
uliza baadhi ya maswali,,,

”kijana tatizo lilikuwa ni nini mpaka mgonjwa
anafikia hali ile mnaendelea kukaa naye nyumbani?
Swali hilo lilionekana ni kama kusifiwa na kipofu
umependeza, hivyo David alikaa kimya kutafakari
huku mawazo yalio kuwa yanaelea kichwani
mwake ni kwamba,,,
”kama nikimueleza kilichotokea baba anaweza
kuwa katika wakati mgumu”
wakati akiendelea kutafakari daktari alimuuliza kwa
mara ya pili na David akajibu,,
”matatizo ya kifamilia tu daktari” ila macho yake
yalionekana kuogopa hivyo yalimfanya daktari
kuhisi kuwa anamdanganya ndipo alipo mchimba
mkwara kutaka kujua ukweli,,
” Kijana haya ni maisha ya mama yako ukifanya
mchezo unaweza ukayapoteza huku unajiona, mimi
natakiwa kuandika taarifa juu ya mgonjwa huyu
unafikiri nitaandika nini? Mama yako ameonekana
ana majeraha sehemu za usoni, hali ambayo hata
wewe unayo hivyo basi mama yako hatopata
huduma nyingine mpaka taarifa zake zitakapo
kamilika pia kumbuka kwamba kwa sasa
ametibiwa kutokana na hali yake kuwa mbaya
lakini bila hivyo tusinge weza kumpokea bila
maelezo kutoka kituo cha polisi na baada ya wiki
mbili anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wake
ukichelewa inabidi asafilishwe kwenda india
gharama zitakuwa juu yenu serikali haito changia
chochote kwa kuwa huu ni uzembe uliofanyika”
Daktari aliongea kwa hasira na kuhamaki.
Maneno hayo yalizidi kumpa wakati mgumu David
maana akifikiria baba anaumuhimu kwake na
mama ana umuhimu kwake nini afanye? Akajikuta
yupo njia panda na chozi jembamba likaanza
kumtoka mtoto wa kiume.
Baada ya mpigano wa mawazo kichwani mwake
akaona bora amueleze tu juu ya tatizo ambalo
limemkuta mama yake ili kuokoa maisha yake.
Daktari akawa anaendelea kuandika maelezo hayo
kwenye faili lake na alipo maliza akamruhusu David
aende nyumbani warudi mchana na chakula
huenda mgonjwa akawa anauwezo wa kupeleka
japo kitu mdomoni.
Daktari alipogeuza macho aliona tangazo lililo
bandikwa ukutani likisema ,,,,,,,
”PINGA UNYANYASAJI KWA WANAWAKE NA TETEA
HAKI ZA BINAADAMU” TANGAZO HILI LIMELETWA
KWENU NA WIZARA YA AFYA IKISHIRIKIANA NA H
ISANI YA WATU WA MAREKANI” Daktari alipo
maliza kulisoma alimwangalia David
ambaye pia macho yake yalilenga kwenye tangazo
lile, Tangazo hilo lilimfanya Daktari kupata wazo
nini afanye juu ya mzee kazinge.
David aliondoka ofisini kwa daktari akiwa na
huzuni huku akifikiria hatima ya wazazi
wake,alifika kwa wenzie ambao walikuwa wa
mesha amka , na macho yao yakigeuka huku na
kule ni dhahiri yalikuwa yana mtafuta David
hatimaye walimuona ameegemea ukutani akiwa
amewapa mgongo,wote walijikuta wakimuita kwa
pamoja David..........!!!!!!
Ndipo mama Coolin alipo nyanyuka kutoka kwenye
benchi na kwenda kusimama karibu naye.,,,
”ulikuwa wapi maana tulikuwa na wasiwasi kuto
kuwepo kwako” aliuliza mama Coolin
David alijikaza na kujitahidi kumjibu japo alikuwa
na kazi ya kuubembeleza moyo wake ambao una
majonzi,alivuta pumzi ya ndani na kumwambia,,,,
”nimetoka kwa Daktari”
”kasemaje ”? Mama coolin aliuliza kwa hofu,
“hali ya mama inaridhisha kiasi tofauti na alivyo
kuja pia anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao
unagharimu kiasi ki kubwa cha pesa kama kita
chelewa ugonjwa ukizidi atatakiwa asafirishwe
kwenda india kwa matibabu zaidi”
Kisha akakaa kimya kwa muda na mboni za
macho yake yakielekea kwenye chumba alicho
mama yake ukimya huo ulimfanya azidi kuduaa
mpaka alipo shtuliwa na kina Stallone ambao nao
walimsogelea,
“Vipi jamani mbona kimya kimezidi kuna
usalama”? aliuliza Junior,
“Kiasi chake upo” mama Cool alijibu,
Baada ya maongezi hayo David aliwaambiwa
waelekee nyumbani huku yeye akianza kujongea.
Na wenzie wakimfuata na safari hiyo iliyoanzishwa
ya kuelekea nyumbani wakiwa kwa miguu ikawa
inasindikizwa na maongezi ya hapa na pale kama
mama Coolin kuwa eleza wenzie kilichojiri kwa
Daktari kama yeye alivyo elezwa na David .
Walichukua muda wa masaa mawili mpaka kufika
njia panda ya mtaani kwao ambayo ndio iliyo
onekana kutaka kuwatenganisha kabla ya kuagana
ili kila mmoja akaendelee na shughuli zake ikiwemo
kupumzika kutokana na uchovu wa usiku kucha,
Davidi alipo taka kuelekea kwao taswira zilianza
kuelea kichwani mwake kwamba kitendo
anachotaka kuki fanya si cha kiuungwana cha
kutaka kuondoka bila kutoa shukrani zake kwa
wema alio fanyiwa na majirani zake alipo kumbuka
usemi mmoja kutoka kwa mwalimu wake
uliosema,,,,,,,
“mwenye busara hujifunza kwa mateso yake” ndipo
alipo thubutu kunyakuwa kinywa chake na kutoa
tabasamu la kirafiki lililosindikizwa na maneno ya
upole yalio mfanya mama Coolin kutoa chozi lenye
mchanganyiko wa furaha na huzuni huku wakina
stallone na junior midomo yao kuonekana kutaka
kusema neno,,,,
“Akili yangu iliyokuwa na upeo mdogo wa kufikiria
leo imeweza kuongezeka baada ya kufikishwa
katika ulimwengu wa faraja ndani ya masaa saba
ya shida, ambayo yalio nifanya niweze kumjua
mwalimu wa maisha na kujua nini maana ya
tatizo, huenda maneno yangu yasisadiki moyoni
kwenu ila naomba mzipokee shukrani zangu za
dhati mimi na familia yangu akiwemo mama yangu
kipenzi,ninyi ni binaadamu mnao stahili kuishi
katika hii dunia”
David alizungumza maneno hayo kwa unyenyekevu
sana ili walio msaidia mpaka mama yake kufika
hospitali wajue kuwa msaada wao unamuhimu na
ameujali kuliko ambavyo wao wangeweza kufikiria
maana wema ni akiba.
Junior nae alizidi kumpa moyo wa ujasiri
kukabiliana na tatizo ambalo lipo mbele yake,,,
“David, thamani ya mtu inakuja pale yeye
mwenyewe anapo jithamini hivyo hatukuwa na
budi kuonesha ushirikiano wetu kwako juu ya
tatizo lako isitoshe sisi ni vijana ambao tuna
tarajia kuja kuwa wazazi wa baade tusipo pendana
na kujaliana matatizo yetu hata watoto zetu
hawato pendana hizi ni changamoto katika maisha
tupo pamoja mpaka mwisho wa tatizo hili.
Upendo huo ulio oneshwa hapo ulimfanya kila
mmoja kujiona ni miongoni mwa watu wema sana
katika dunia maana kila mmoja alitambua thamani
ya mwenzie.
mama Coolin pia aliweza kuahidi kuandaa chakula
cha mgonjwa hivyo aliomba aruhusiwe awahi
kukipika, basi wote wakakumbatiana na kila mmoja
kuelekea kwake.
*****************
Ukimya ulio tanda kwenye nyumba ya kina David
ulimuogopesha sana na akiangalia milango yote
imefungwa jukumu la kuanza kuita lika chukua
nafasi mdomoni mwake,,,
Baba!!!!!!? Baba!!!!..,? nisha !!!!!? Lakini bila
mafanikio zaidi ya sauti zilizo kuwa zinajirudia
rudia kumkera tu maskioni mwake ghafla alishtuka
alipo vutwa shati kwa nyuma na shingo yake ilipo
geuka kumbe alikuwa ni Dasoni hakuwa na budi
kuitoa ile sura yenye mikunyanzi usoni mwake na
kumbeba mdogo wake kipenzi,
Alipo taka kumuuliza nisha yuko wapi macho yake
yaliweza kumuona kwa mbele Nisha akija huku
akiambatana na mama Muksini, walipo wasili
karibu yake mama Coolini alimueleza,,,,,
“milango niliifunga jana baada ya nyie kwenda
hospitali baba yako tulimpeleka kwa mwenyekiti
hivyo alilala huko kutokana na pombe alizo
kunywa na huu mguu tulikuwa tunaelekea huko ila
Dasoni ndiye alie wahi kukuona wakati ukija hapa
ndio maana akakukimbilia”
Alipo maliza aliuliza hali ya mgonjwa na jibu likawa
lilelile alilo wapa wakina mama Coolin.
“Basi tuongozane twende wote huko”David
alimueleza mama Muksini,
“David jihurumie na wewe ungeoga kwanza kisha
uendee nyumbani kwangu Yule masichana wangu
wa kazi akupatie chai ndio uje maana hiyo kesi
haiwezi kuendeshwa bila wewe kuwepo”mama
Muksini alimueleza David baada ya kumuhurumia
lakini kwa David haikuwa hivyo,,
“nashukuru sana kwa ukarimu wako lakini kiukweli
sina hata hamu ya kula kitu chochote kile kwa
sasa ni vyema tuwahi huko kwa mwenyekitini ili
tujue kinachoendelea huenda hata yeye Baba
akawa na wasi wasi juu ya hali ya Mama”
Mama Muksini kutokana na maelezo ya David
akawa hana kipingamizi ikabidi waongozane
kuelekea kwa mwenyekiti na walipo anza kuiona ile
bendera ya chama cha mapinduzi (ccm) iliyo
chakaa ikipepea juu ya mlingoti David alifanikiwa
kumuona Baba yake akiwa na mwenye kiti
wakitoka ndani kwenda kwenye mabenchi ambayo
wakina mzee Nyomolage walisha wasili kitambo
huku akiwa amesha funguliwa zile kamba alizo
fungwa usiku na pombe zilisha kwisha kichwani.
Moyo wa hasira ulimshika David alipo kumbuka
hali ya Mama yake kule hospitalini lakini alijikaza,,,
Miguu yao ilipo kanyaga eneo lile macho makavu
ya David yalionza kubadilika rangi kutaka kuwa
mekundu kutokana na hasira yalipo gongana na
mzee Kazinge ana kwa ana na moyo wa mzee
kazinge ukionekana kuteseka na aibu kwa kitendo
alicho kifanya maana Alisha elezwa yote yalio
tokea na mwenyekiti wakati walipo kuwa
wanajibizana akiwa anafunguliwa zile kamba alizo
fungwa.
Bila kuchelewa ndugu mwenyekiti akaanzisha kikao
na swali kwa David juu ya hali ya mgonjwa
kwanza.. Jibu alilo toa David lilizidi kuchokonoa
aibu iliyo jificha kwa mzee kazinge kufikia hatua ya
kuinama chini lakini mwenyekiti aliendelea kuuliza
maswali mengi mengi ambayo yalichukua muda
mwingi mzee Kazinge kuya jibu mpaka ilipo timia
saa saba kasoro hakuna jibu wala sababu ya
msingi ambayo iliyomfanya mzee kazinge kumpiga
David na mkewe.
Mwenye kiti ndipo alipo amua kutaka kukata shauri
kwa kuruhusu mzee Mazinge apelekwe kituo
kidogo cha polisi kwa matatizo aliyo msababishia
mkewe mpaka kulazwa.
Kutokana na hatua aliyofikia mwenyekiti ilimtisha
mzee Kazinge alipofikiri kuiacha familia yake kwa
mara ya pili tena kwa ujinga , na yeye kwenda
gerezani, kilimuumiza sana na kuleta mlipuko
mkubwa wa mamumivu mwilini mwake na chozi la
kujilaumu likaanza kumtoka hali ambayo ilileta
huzuni kubwa kwa kina Dason na Nisha,.
Ali watazama na kufikiria kama mkewe atakufa
hospitali ni zahiri safari hii ataukumiwa kifungo
cha maisha.ndipo macho yake yalipomtazama
David kisha kugeukia upande wa kina Nisha na
Dason ambao walipakatwa na mama Muksini kisha
kuanza kusema,,,,,
“Mwenyekiti kwanza naomba radhi kwa niliyo
yafanya naamini kwangu ni hasira na pombe
ambazo ndizo zilizo nifanya nitende hivi, pia familia
yangu ambayo naipenda sana najua ni vigumu
kuomba radhi kwenu lakini naomba mnisamehe pia
mkaniombee msamaha kwa mama yenu maana
nikienda kituoni huenda nisionane na nyie tena
wala mama yenu.
“ Kikubwa ni kwamba familia hii sio maskini ila
kuna mambo ambayo yamejificha leo ninge penda
kuwa eleza zile kumbukumbu ambazo niliapa
hazito saulika katika maisha yangu yote David
najua unajua ulicho kiona kwa macho yako ila
chanzo hukijui. Tega sikio ili ujue kwanini
nilikukataza usiendee mjini kwa wakati huu. Wote
walijikuta kukaa kimya huku macho na maskio ya
David yakikaa kiudadisi kutaka kujua chanzo
Mzee kazinge anaanza kuwa simulia,, ilikuwa
mwaka 2002
Ilikuwa mwaka 2002 ndani ya jiji la dar es saalam
nikiwa mfanyakazi katika NMB banki iliyopo tawi la
magomeni katika kitengo cha mikopo, kitengo
hicho kilinifanya nifahamiane na watu wengi sana
na wenye tabia tofauti kutokana na ukalimu nilio
nao.
Japo niliiamini kuwa hata uwe mwema kiasi gani
lazima utakuwa na maadui wanao kuzungua, hao
pia nili jitahidi kuishi nao.kila ofisi utakayo kwenda
kama ikiwa na wafanyakazi thelathini basi kumi na
watano lazima walikuwa wanalifahamu jina la
Alfred Kazinge
Miaka ilivyozidi kwenda huku nikiwa tayari nina
watoto wa wili David na Nisha, jina langu
lilijulikana zaidi ndani na nje ya jiji la dar es
saalam hasa na wafanya biashara waliokuwa
wanaingia na kutoka. nilikuwa na pokea simu
nyingi sana kiasi ambacho zingine zikawa zinaleta
ugomvi kwa mke wangu magrety .(mama david)
Umaarufu huo ulianza kuniletea dosari katika kazi
yangu baada ya kumpata rafiki Helman ambaye
ndio nikamfanya ndugu yangu wakaribu baada ya
kuhamia hapo jijini dar es salaamu kutokea mkoani
Tanga ambapo ndipo walipo baadhi ya ndugu
zangu. Na makaburi ya wazazi wangu yalipo.
Bwana Helman alianza kunifanya nichelewe kurudi
nyumbani kwangu kwa kunipitisha sehemu nyingi
za anasa na kunikutanisha na marafiki zake ambao
wengi walionekana ni wenyeji wa Arusha,.kila
walipo kaa walikuwa wanazungukwa na wasichana
ambao nilikuwa nashindwa kuwaangalia kwa mara
ya kwanza kutokana na nguo zao za anasa walizo
kuwa wanavaa.
Hivyo sehemu hizo za starehe zilinifanya
kumgeuza mke wangu magrety kuwa mlinzi wa
nyumba na mtunza muda kwa kuangalia saa ya
ukutani ni saa ngapi narudi na alipo sikia honi ya
gari majukumu ya kufungua mlango pia aliyabeba
na alinivumilia sana hata nilipo amia dunia
nyingine yenye utembeaji wa kupepesuka( ya ulevi)
ITAENDELEA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni