Sehemu ya kwanza
Jua lilikuwa likiaga upande wa mashariki na
kwenda kuungana na magharibi ili kukamilisha
siku, huku likisindikizwa na hali ya hewa yenye
ubaridi kwa mbali. Ndege pia walipeperusha
mbawa zao kutafuta makazi ambayo yatawafanya
walione jua la kesho hata baadhi ya nyumba za
jirani zilionekana kufuka moshi kama ishara ya
maandalizi ya chakula cha usiku. Sauti za wakina
mama pia zilisikika zikiwaita watoto wao kurudi
nyumbani ili kuepukana na dhoruba za giza
litakapo kuwa kubwa, wengine wakiwatuma
wakubwa kwenda kununua mafuta ya taa na
mishumaa ili waweze kupata mwanga.
Lakini nyumba ya kina David ambayo ndio ilikuwa
ikionekana yenye thamani katika kijiji hicho cha
Gairo mkoani Morogoro ilikuwa tofaauti baada ya
kuzongwa na huzuni pamoja na mabishano ya
hapa na pale juu ya swala la David kutaka kwenda
mjini baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha
sita katika shule ya sekondari Gairo.
Familia ilikuwa imekusanyika katika kitanda cha
mama yao mzazi, ambaye alikuwa hoi kutokana na
maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa
muda mrefu. Yaliyo sababishwa na mshtuko
alioupata baada ya kupata taarifa juu mbaya,
kuwa mumewe kahukumiwa kifungo, kutokana na
ubadhirifu wa fedha uliotokea katika benk ya NMB
tawi la magomeni. Tawi alilokuwa akifanyia kazi
miaka ya nyuma huko kwenye jiji la maraha na
uchafu wote Dar es saalam.
“swala hili halitowezekana hata kidogo. Ni bora ya
hawa wadogo zako ndiyo wangelilia kwenda mjini
lakini sio wewe. Kwani kumbukumbu unazo za nini
kilichotokea huko unakotaka kwenda, mimi Mzee
Kazinge baba yako nasema kauli ya mwisho baki
hapa kijijiniâ€
Baada ya kumaliza kuongea kwa jazba na hasira
mzee Kazinge alitoka nje.
“Baba!! Baba!!...â€.David alimuita baba yake kwa
sauti ya unyenyekevu lakini mzee huyo hakugeuka
nyuma.
David alimwangalia mama yake kwa huzuni sana
kisha akamueleza,,,,
“Mama safari hii ni kwa sababu yako huenda
nikafanikiwa kupata pesa huko zitakazo saidia
kufanikisha kufanyiwa upasuajiâ€
“Najua mwanangu kama unanipenda mama yako.
Unatamani niendelee kuishi. Lakini fikiria pia kama
utaondoka hapa hakuna wa kunihudumia, wewe
ndio tegemeo langu , baba yako mwenyewe hali
yake ndio hiyo unayoiyona tangu ametoka jela
amechanganyikiwa pombe ndiyo imekuwa furaha
yake, nakuomba ubaki baba yangu kama Mungu
amepanga niiishi nitaishi lakini kama hakupanga
basi kazi yake haina makosaâ€
Mama yake aliendelea kumsisitizia;
“…Lingine wadogo zako atawahimiza nani kusoma
na kuwatunza pia�
Lakini David hakujibu swali hilo, badala yake
alibaki kimya tu anamuangalia mama yake
aliyekuwa anazungumza kwa shida kitandani.
Maneno hayo yalimuumiza sana David machozi
yakamtoka lakini alijikaza kiume. Hasa baada ya
kuona wadogo zake wamenyong’onyea na kukosa
amani ndani ya mioyo yao. Kutokana na maneno
aliyoyasema mama yao na malumbano yaliokuwa
yakiendelea hapo ndani, ndipo alipo wavuta na
kuwapakata na kuongea nao.
â€Msijali wadogo zangu mimi sitaondoka na wala
mama hatokufa alikuwa anatania tu sawa Dason ?
“Ndiyo†Dason aliyekuwa mdogo wake wa mwisho
alijibu
“Nishaaa?â€
“Abee
“Haya nendeni jikoni mkaandae mimi nakuja kupika
sawa�
“Sawa kakaâ€.alijibu Nisha mdogo wake wa pili
Mzee Kazinge alivyotoka alielekea kilabuni ambako
wanauza pombe za kienyeji ili kukamilisha furaha
yake. Alirudi usiku akiwa amelewa chakari,
alipokuwa njiani aliropoka maneno ambayo
yalionekana kuendana na ukweli wa maisha yake.
â€Elimu yangu mwenyewe imenipeleka gerezani!
Nimekosa nini katika nchi hii, kipi bora kuwa
mjinga au kuwa na elimu? Ama kweli Serikali ina
siri kali!!!â€
Aliongea maneno hayo njia nzima mpaka alipofika
nyumbani kwake. Familia yake ilikuwa imesha lala
baada ya kupata chakula cha usiku ambacho
kiliandaliwa na David, wakati huo ilikuwa yapata
kama mishale ya saa nane usiku hivi. Kijiji kizima
kilikuwa kimya, sauti yake iliweza kuamsha baadhi
ya majirani. Aligonga mlango wa nyumbani kwake
zaidi ya mara nne lakini hakuna alieitika. Ndipo
alipozunguka nyuma ya nyumba na kumgongea
David dirishani.
â€David, Davidâ€
â€Naam†sauti yenye usingizi iliitika.
â€Mimi nagonga we husikii eeh?â€
“Nakuja babaâ€
Ndipo alipo nyanyuka kitandani na kwenda
kufungua mlango. Ghafla David alijikuta akipokea
kipigo kutoka kwa baba yake,,,,
†Mimi na wewe nani baba humu ndani eeh?â€
Alimuliza David huku akiendelea kumpiga.
â€Haiwezekani mimi nigonge mara zote hizo wewe
upo ndani kama ndiye mwenye nyumba hiiâ€
Hasira hizo pia ziliendana na swala la David
kutaka kwenda mjini maana alilihusisha pia wakati
kipigo kikiendelea,,,,,,
“Unataka nikuzike mapema huko unakotaka
kwenda?â€
â€Unajifanya hujui kilicho mfanya mama yako aje
huku kijijini wakati niko gerezani?â€
Bila kujibiwa aliendeleza kipigo ambacho kilimfanya
David aanze kuhisi maumivu mpaka kufikia hatua
ya kulia kwa sauti kubwa kama mtoto mdogo
wakati ni dume linalo kimbilia miaka ishirini na
ushehe.
Kilio cha David, kiliwatoa majirani majumbani
kwao. Mama yake alipokisikia kilio cha mwanae,
alijitahidi kwenda kumuamulia japo alikuwa hoi,
kama ilivyo misemo ya Waswahili samaki mmoja
akioza wote wameoza mama yake naye
akajumuishwa katika kipigo hicho bila kujali afya
yake.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa mama David mpaka
majirani walipo wasili eneo la tukio na kumshika
mzee Kazinge.
â€Jamani muwaisheni hospitali haraka huyu mama.â€
Sauti za watu zilisikika huku wengine
wakimbembeleza David.
â€Mwenye namba ya gari la hospitali apige upesi
bila hivyo tutachelewa†wazo lilitolewa na
kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na baada ya
muda gari likaletwa.
Nisha na Dasoni pia waliamka baada ya zogo
kuwa kubwa. Walijikuta wakilia bila kujua kinacho
endele kutokana na umri wao, japo Nisha alikuwa
kigoli na Dason ni mdogo asiye pungua miaka tisa.
Mwana mama Muksini ambaye alikuwa wa
makamu alipowaona aliwafuata na kuwachukua
kisha kumuongezea kanga nyingine. Kwani Nisha
maumbile yake yalikuwa yameanza kuonekana
hasa nyonga na chuchu zilizo chongoka kwa kuwa
alitoka na kanga aliyo lalia tu. .
â€Sasa jamani huyu mzee Kazinge tumpeleke kwa
mwenyekiti wakati mkewe akiwaishwa hospitaliâ€
Alizungumza mzee Nyomolage.
Safari ikaanza baada ya kujigawa makundi mawili.
ambayo ni mzee Nyomolage, na mama Muksini
akiwa na kina Dason na mzee Mtepa pamoja na
mzee Kazinge mwenyewe wao walielekea njia ya
kwa mwenyekiti lakini kwa kumshikiria mzee
kazinge asije akawakimbia na pombe zake alizo
kuwa nazo kichwani.
David,Stallone,Junior na mama coolin wao
walielekea hospitali kumpeleka mama David.
Safari ya kwa mwenyekiti haikuchukua muda
maana hapakuwa mbali sana na kwa kina David
ndani ya dakika kadhaa wakawa wamewasili na
mzee Nyomolage ndie aliyegonga mlango......
â€mwenyekiti,,mwenyekiti†sauti mbili tu zilitosha
kumuamsha mzee maige ambaye ndie alikuwa
mwenyekiti.
Mwenyekiti aliamka na kutoka nje akiwa amebeba
taa ya chemli iliimsaidie kuona kutoka na kuto
kuwa na umeme nyumbani kwake.
â€Vipi jamani mbona usiku na mkusanyiko mkubwa
kuna nini!!? Aliuliza mwenyekiti kwa mshangao,
Mzee Nyomolage alionekana kuwa kiongozi wa
msafara kwasababu alikuwa jirani sana na mzee
kazinge hivyo swali hilo alijibu yeye,,,,,
â€tumemleta mzee Kazinge alikuwa anawafanyia
vulugu familia yake na hivi tuna vyoongea mkewe
amewaishwa hospitali hali yake si nzuri ndugu
mwenyekitiâ€.
â€Mzee Kazinge tatizo nini mpaka unaleta vulugu
kwa familia yako eeh? Mwenyekiti aliuliza
â€umesha sema familia yangu nyinyi inawahusu nini
mbona mnakuwa wa mbea kuingilia mambo yasio
wahusu? We mwenyekiti si umelala na familia yako
nani aliyekuja kuku uliza kwa nini umelala eeh ni
jibu sasa�
Majibu ya mzee kazinge yalionekana dhahiri
kutoeleweka kutokana na pombe aliyokuwa
amekunywa iliyo mlewesha kufikia hatua ya
kutojua anazungumza nini na mbele ya nani.
†Mzee Nyomolage na wenzio embu mfungeni
kamba kisha muingizeni ndani mpaka kesho
panapo majaaliwa pombe ikiwa imemusha
kichwani tutaendelea na mshauri hayaâ€alizungumza
mwenyekiti.
Zoezi hilo likafanyika kwa haraka.
â€Ndugu mwenyekiti basi na mimi naomba watoto
hawa wa mzee kazinge nikalale nao maana kwao
hakuna mtu kaka yao pia ameelekea
hospitaliâ€.mama Muksini alionesha huruma kwa
watoto hao Nisha na Dason
â€Hakuna shida mama ila kesho mjitahidi kuwahi
ilitujue tunafanya nini juu ya tatizo hili.
â€Sawa na shukuru tutajitahidi†alijibu mama
muksini kwa heshima.
Muda huo huo mzee Nyomolage na wenzie
walielekea majumbani kwao na ilikuwa yapata
kama saa kumi kasoro hivi,njia nzima mazungumzo
yalikuwa juu ya swala hili.
*************
Watu walionekana wakipisha barabarani baada ya
kusikia king’ola cha gari la wagonjwa lililokuwa
mwendo kasi likiwasili katika eneo la hospitali ya
wilaya Gairo,pilika pilika za manesi zilifanyika kwa
haraka, kitanda chenye matairi kiliandaliwa
hatimaye mama David alishushwa kwenye gari na
kulazwa kwenye kitanda hicho,mbiombio
kilikimbizwa kuelekea icu (chumba cha wagonjwa
mahututi) maana hali yake ilionekana kuwa mbaya
zaidi.
.David hakuwa mbali nae alijipa majukumu ya
kusukuma kitanda hicho, macho ya David yalikuwa
kwa mama yake na sala nyingi zilimtoka ndani ya
moyo wake,
Kwakuwa moyo wake ulikuwa na uchungu usio
stahimilika kinywa chake kilitoa maneno ya
majonzi mbayo huweza kupekecha mwili na moyo
wa mtu yeyote yule mwenye roho ya kibina
adamu.
â€Dokta jitahidini kuokoa maisha ya mama yangu
jamaniâ€
â€mama usituache wenyewe,tutakuwa kimbilio la
nani sisi�
â€Nisha na Dason wana kusubiri nyumbani nitakuwa
sina cha kuwaeleza ukiondokaâ€
Maneno hayo aliyokuwa anaya zungumza David
kwa sauti ya kuchoma moyo, yaliwafanya watu
waliyo yasikia kushika vifua vyao na kutingisha
vichwa vyao kusikitika kwa huruma
Baada ya mwendo wa mita kadhaa wakawa
wamefika kwenye chumba cha wagonjwa
mahututi .
Mmoja kati ya wauguzi alimzuia David asiingie
katika kile chumba na kumwambia,
â€kijana usijali tutajitahidi kuokoa maisha ya mama
yako hivyo subiri kwenye benchi.†Aliketi lakini
aliendelea kulia kilio cha kwikwi hata maumivu ya
kipigo akawa hayasikii zaidi ya uchungu uliokuwa
ukitapatapa ndani ya moyo wake juu ya mama
yake.
Muda huo huo jamaa zake ambao walibaki kwenye
dirisha la mapokezi kutoa maelezo pia walifika
eneo alilokuwa David na kumfariji.
***************
.
Ndani ya chumba cha matibabu mama David
alionekana kupoteza fahamu hivyo ikabidi
wamshutue na kifaa maalumu, mipigo mitatu tu
ilitosha kurudisha fahamu yake hata vidole vyake
vilivyokuwa vimejikunja vilianza kutikisika na
kujikunjua taratibu,
Dokta aliyekuwa anaongoza jopo hilo la madaktari
walio kuwa wamevaa nguo sale zenye rangi ya
kijani na vikofia kichwani na kujifunga vitambaa
midomoni , alishusha pumzi baada ya kuona
graphu ya mapigo ya moyo inasoma ipasavyo
kwenye komputa , hata wenzie pia walishusha
pumzi juu ya zoezi hilo gumu la kumrudishia
fahamu mama David
â€mungu mkubwa jamani†sauti ya dokta wa kike
ilisikika.
Lakini hata hivyo upumuji wake ulikuwa sio wa
kawaida ilibidi awekewe mirija maalumu
iliyounganishwa na hewa safi ya oksijeni ambayo
itamsaidia kupumua kwa muda mpaka hali yake
itakapo kuwa nzuri.
madaktari walipo maliza wakawa wanakusanya
vifaa vyao na kuhakikisha mgonjwa anaachwa
katika hali inayo ridhisha na chini ya uangalizi wa
manesi kisha kwenda kuendelea kutoa huduma
kwa wengine.
************
Sauti za Ndege zilianza kusikia na kijua chenye
miale myembamba iliyokuwa inapigana
kufukuza giza la alfajri kilianza kuchomoza, watu
wengi walio lala kwenye mabechi ya hapo hospitali
walianza kuamka,na wengine wakipishana kwenda
kwenye vyumba vya wagonjwa wakiwa wameshika
vitafunwa na chupa za chai,.wafagizi pia
waliendelea na usafi.ilikuwa yapata majira ya saa
kumi na mbili asubuhi ,
David alikuwa amejiinamia chini kwenye benchi
ambalo lipo kaaribu na chumba alicho kuwa mama
yake, majirani walio msindikiza walikuwa
wamepitiwa na usingizi kutokana na uchovu.
Kama ilivyo ada uchungu wa mwana ana ujua
mzazi hivyo David hakuwa na budi kujua uchungu
wa mama yake pia, uchungu huo ndio ulimfanya
kukosa hata lepe la usingizi,
.kichwa kilicho kuwa kimeinama chini kilinyanyuka
baada ya kushtuliwa na mlango wa chumba alicho
lazwa mama David, miguu ya David ilichanganya
kumfuata yule daktari aliye toka mle ndani na
kumshika koti lake na maneno yalio kuwa yana
muelemea moyoni mwake yaka mtoka,,,,,,,
â€Daktari mama yangu anaendeleaje? tafadhali
usinifiche,,
Daktari alimtoa mikono David kisha kumshika
begani na kumueleza........
â€hali ya mama yako inaridhisha kiasi ila kuna
mambo inabidi tukazungumzie ofisini kwanguâ€
Walifuatana mpaka ofisini na dokta alianza kumu
uliza baadhi ya maswali,,,
â€kijana tatizo lilikuwa ni nini mpaka mgonjwa
anafikia hali ile mnaendelea kukaa naye nyumbani?
Swali hilo lilionekana ni kama kusifiwa na kipofu
umependeza, hivyo David alikaa kimya kutafakari
huku mawazo yalio kuwa yanaelea kichwani
mwake ni kwamba,,,
ITAENDELEA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni