Baada ya
mahusiano ya miaka minne ya uaminifu na upendo kwa binti mmoja hivi jina
kapuni, ndipo safari yangu ya kuto mwamini tena mwanamke katika
mahusiano ilipoanzia kutokana na kile alichonifanyia.
Katika maisha
yangu ya mahusino na huyo binti, nilikuwa mwaminifu sana pia nilimwamini
kupita kiasi, siwezi sema labda sikuwa na uzoefu wa muda mrefu katika
mapenzi laahasha, nilikuwa na uzoefu wa kutosha kuliko hata binti
mwenyewe.
Kutokana na
mazingira aliyokuwa ameyajenga kwangu ndio kilikuwa kichocheo kikubwa
kilicho changia kumwamini kupita kiasi, Kwa uaminifu niliokuwa nao hata
kama ungempiga picha akiwa nyumba ya kulala wageni(guest) ukaniletea
ningekupinga kwa nguvu zote na kukuambia ni photo shop hiyo, unaweza
kujiuliza labda alikuwa ananipa nini laahasha utajiumiza kichwa kwa
kujiuliza maswali, maana kama ni mapenzi nilikuwa mkongwe kabla yake na
nilikutana na wanaoyajua na kuyamudu hayo mambo ya kiutu uzima. Katika
mapenzi binti alikuwa ni mgeni sana vitu vingi nilimpatia mafunzo kwa
vitendo.
Kilicho kuja
kubadilisha mtazamo wangu katika swala la uaminifu ilikuwa ni siku moja
alipokuja kwangu, basi wakati nimekaa nae yapata mida ya saa nane mchana
kuna mtu alikuwa anapiga simu yake, yule binti akawa hataki kupokea
baada ya jamaa kukazana kupiga kama mara tatu nne hivi huku simu
haipokelewi, ikanibidi nimuulize binti swali kwanini hapokei na ni nani
ane mpigia, hapa nikapewa jibu jepesi, kwamba kuna jamaa anamtaka hivyo
huwa anamsumbua kwa kumpigia simu, nikamuuliza swali la pili, je ulisha
wahi kumwambia uko katika mahusiano, nikajibiwa ndiyo,haikupita muda
akapiga tena nikapokea jamaa hakuongea baada ya kusikia sauti ya kiume,
nikaamua kuishia hapo maswali yaliyo baki nikawa najiuliza mwenyewe na
kujijibu.
Njia ya muongo
ni fupi sana na siku zote ukiwa muongo usiwe msahaulifu, ilikuwa ya pata
saa moja jioni kile kigiza cha usoni, nikaamua kwenda kuoga nikamuacha
akiwa amejilaza kitandani, baada ya kufika bafuni nikagundua nimesahau
sabuni chumbani, nilipofika mlangoni nikasikia kama binti anaongea na
simu basi nikafungua mlango taratibu kwa kunyata kwa vile chumbani
nilikuwa sijawasha taa kulikuwa na giza hivyo hakuweza kuniona.
Baada ya
kuingia chumbani nikagundua alikuwa anaongea na yule jamaa aliekuwa
akimpigia ile mida ya saa nane mchana, huku akimuuliza mbona ulikuwa
haupokei simu na ninani aliepokea simu yako, binti alijitetea sana huku
akimwambia ni binamu yangu, ulipopiga simu nilikuwa nae hivyo akasema
ngoja leo akuzengue. Akamalizia na neno moja kwamba naomba uniamini.
Nilivuta pumzi
nikapiga konde moyo nikingojea wamalize maongezi yao, baada tu ya
kumaliza maongezi nikamuuliza binamu umemaliza kuongea, alishikuta sana
alipogundua kwamba nilikuwa chumbani na nilisikia kila alichokiongea,
alilia na kuniomba msahama, sikumsamehe kwa siku hiyo baada ya majuma
mawili ya kujitafakari nikaamua kutoa msamaha, tukaendeleza safari yetu
ya mahusiano iliyokatika behewa moja la uaminifu, likawa limesalia moja
tu la upendo. UPENDO BILA UAMINIFU.
Basi hapo ndiyo mwanzo wangu ulipoanzia mpaka leo hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni