Jumanne, 2 Juni 2015

MAMA CHANGAMOTO ALIZOPITIA HADI KUFANIKIWA.









"Naitwa Zuwena Hassan Kasweba ni mzaliwa wa Kigoma Mwanga majengo.
Wakati naingia rasmi katika shughuli hii ya ujasiriamali nakumbuka sikuwa na mtaji na hakuwepo mtu wa kunisaidia kupata mtaji ili niweze kuanzisha biashara yangu na wakati huo nafikiria kuanzisha biashara mume wangu wa ndoa ambae mpaka sasa bado nipo nae hakutaka kabisa niwe mjasiriamali ingawa uwezo wa yeye kunipatia mtaji alikua nao kwani alikua ni mfanyakazi katika shirika la mtu binafsi na alikua akilipwa vizuri kiasi kwamba angeweza kunisaidia ila hakua akitaka mimi niwe mjasiriamali namimi nilimsikiliza kwa heshima ya ndoa na kujali maamuzi yake japo kua sikupenda kua nashinda nyumbani bila shughuli yoyote ya kufanya ila sikua na jinsi.

Nakumbuka mwaka 2012 sehemu ambayo mume wangu alikua akifanya kazi katika lile shirika kulitokea wizi kwa wafanyakazi na baadhi ya wafanyakazi walisimamishwa kazi katika hilo shirika mume wangu nae alikuwemo katika kundi hilo la wafanyakazi walio simamishwa kazi ikabidi uwepo tu nyumbani huku akihangaika kupata kazi sehemu nyingine
wakati huo yupo nyumbani bado hajapata kazi nyingine ya kumuingizia kipato tulikua tukitumia pesa za akiba tulizokua tukiwekeza wakati yupo kazini hatimae pesa zikawa zinaelekea kumalizika
Nafikiri hapa ndipo ujasiriamali wangu ulipo anzia, kwa kua alikua hayupo tena kazini na yeye ndio kichwa cha familia tuliekua tunamtegemea nilichokifanya ni kumuomba tena anipe nafasi ya kufanya biashara ili tusaidiane kulea familia nashukuru mume wangu alinielewa kwa hili.
Ndani tulikua na Shillingi Laki Mbili katika zile pesa za akiba zilizobakia nikamuomba mume wangu nijiazime Shillingi Laki mbili ili nifanyie mtaji wa biashara ninayotaka kuanzisha pindi biashara itakapo changanya nitazilipa ili zirudi katika bajeti ile ile iliyokuwepo ya akiba ndani akanikubalia.
Biashara niliyotaka kufanya ni biashara ya uuzaji wa vitenge kwa kua nilikua na mama yangu mdogo alikua akiifanya hii biashara na ilikua inamlipa sana
Nikaanza kua nachukua vitenge vya WAX Original kutoka Congo Soko la Kigoma mjini nakuja kuviweka nje ya nyumba yetu kwa kuvitandaza nilikua nanunua kwa bei ya jumla. Kila kitenge kimoja nanunua Shillingi 14,500 nauza kwa Cash Shillingi Elfu 30,000 faida napata shillingi 15,500 nikawa na hesabia faida elfu15 zile miatano miatano nikawa nahesabia gharama za usafiri kila nikiuza kitenge kimoja elfu kumi naweka katika kibubu elfu tano tunatumia nyumbani wakati huo pia nilikua nakopesha vitenge hivyo ila nilikua nakopesha kwa kubandikisha kwa maana ukikopa kila siku unabandikisha elfu mbili mpaka deni lako litakapo kwisha nilikua nakopesha kwa shillingi 35,000 mwezi mmoja
Namshukuru mungu biashara ilikua na nikafanikiwa kulipa ile laki mbili na nikafanikiwa kupata Fremu ya kukodisha nikahamisha biashara yangu katika fremu (duka) biashara ikawa inaendelea vizuri
Kwa bahati mbaya fremu ile ikavamiwa na majambazi usiku na kuchukua mzigo wote wa vitenge na kulikua na pesa sikuzitoa siku hiyo vyote vikachukuliwa
Nikaanza kuyumba sasa katika biashara hali ikawa sio nzuri pesa kidogo niliyokua nayo nikanunua tena mzigo lakini haukua mkubwa
Kwa bahati nzuri mume wangu alikua mjuzi sana wa kutumia mitandao ya mawasiliano aliwahi kuona Tangazo moja kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Taasisi ya FOCUS VICOBA kua wanatoa mikopo ndani ya dakika 55 kwa kwenda katika ofisi zao dar es salaam au unaweza kujiunga mtandaoni (ONLINE) katika tovuti yao na ukapatiwa mkopo
Kwa kua tulikua tupo mbali Kigoma hatukua Dar es salaam ikabidi tujiunge katika tovuti yao tuliipata hii tovuti yao hii hap tukajiunga na kupatiwa mkopo tuliomba mkopo wa Million 5 tukiamini tunaweza kuulipa
Tulijiunga na FOCUS VICOBA katika hii tovuti  na kupewa mkopo
Nikaendelea na biashara yangu ile ile ya vitenge kupitia mkopo tuliopata VICOBA mpaka leo biashara inaendelea vizuri na mkopo tumeshaulipa maisha kidogo yanakwenda nina maduka matano kigoma mjini na Dar es salaam yapo matano pia nimefungua mgahawa wangu anasimamia mume wangu upo mbezi luis. Namshukuru mungu kwa kweli"
MWISHO WA KUNUKUU.
Nini maoni yako juu ya mama huyu? Kipi umejifunza kutoka kwake?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni