Jumamosi, 16 Mei 2015

Wambura Mfungwa



INASISIMUA NA KUTISHA ILA
INAFUNDISHA
Katika kijiji cha Matare wilaya ya
Mugumu
Serengeti, bwana Wambura
alikamatwa kwa kesi
ya kusingiziwa na kuhukumiwa
kwenda jela
miaka mitatu. Huku nyuma akiacha
mke na
watoto wanne waliokuwa wanasoma.
Hukumu
hiyo ilimtesa sana kichwa chake,
alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa
aingie katika
moyo wake na kuupata ukweli. Alilia
na
umaskini wake, labda angepata wakili
mzuri
angeweza kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda
gerezani huku akiumia sana rohoni.
Aliyaanza
maisha mapya kwa shida sana,
akawamnyonge
kila mara na mwili ukapoteza afya
kiujumla.

Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki
aliyekuwa na cheo ama jukumu la
uzikaji wa
wafungwa hasahasa ambao
hawakuwa na ndugu
ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale
gerezani. Mzikaji alijaribu sana kumtia
moyo
Wambura na kumwaminisha kuwa
hiyo ilikuwa
hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja
ukweli
utajulikana tu! Bwana Wambura
maneno ya
mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea. “Siwezi kuvumilia
kukaa
gerezani miaka mitatu…..kama unajali
kilio
changu nisaidie nitoroke kwa namna
yoyote ile
ndugu yangu!!” Wambura alimsihi
mzikaji.
SIKU MOJA mzikaji akamwambia
Wambura kuwa
msaada umepatikana. Lakini yataka
moyo!!
“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
nitoke
humu!!” alijibu kwa msisitizo huku
akimtegea
sikio mzikaji. “Msaada pekee wa
kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
yaani
mfungwa akifa mimi nakuunganisha
naye
kwenye jenerza…..” akashusha pumzi
kisha
akaendelea “Wewe ukisikia kengele ya
msiba,
njoo mara moja kwenye chumba cha
maiti,
utakuta tayari sanduku liko katikati ya
chumba
linakuwa halijafungwa, funua mfuniko
ingia
ndani yake ulale pembeni ya maiti
kwani
sanduku huwa kubwa la kutosha kila
aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia misumari.
Baada ya
muda tutalipakia kwenye gari na
kutoka kwenda
nje ya gereza makaburini
nikiongozana na
baadhi ya wafungwa na maaskari
magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi
30 nitarudi kukufukua. Hautaweza
kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
lilimtisha
sana Wambura. Hata hivyo akaona
afadhali
afanye hivyo
kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa. Siku moja akasikia kengele
ya msiba.
Akafanya kama alivyoelekezwa na
mzikaji.
Akaenda na kuingia chumba cha
maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya
maiti
iliyokuwepo. Mara akasikia mtu
ameingia na
kulipigilia msumari sanduku. Muda
mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na
kuwekwa
kwenye gari. Gari likatoka nje ya
gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia
japo hofu
ilizidi kutanda. Alimtegemea sana
mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa
maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!!
Dakika
thelathini kimya. Joto nalo likazidi
kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…” alijisemea
kisha
akajiongezea kauli ya ujasiri.
“Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka
mitatu
kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini
zinishinde” KWA kuwa alishakaa
gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua aliyekufa
ni nani…
ni kweli aliogopa kuitazama maiti
lakini aliona
kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
Akaifunua
upande wa usoni… Kwa kuwa
kulikuwa na giza
nene alikodoa sana macho
kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
AMEZIKWA NA
AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu
katika maisha
yako, kwanza ni dhambi!! Pili
mwanadamu
anakumbana na vikwazo kama
unavyokumbana
navyo wewe hadi kumwendea yeye.
Hivyo
kumpatia maisha yako ni kuzidi
kuyaweka
hatarini zaidi!!
Umeonewa umesingiziwa
unanyanyaswa…..
mwachie Mungu afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua
naye ni
maiti…… tazama mateso
atakayoyapata hadi
kufa kwake…..Bila shaka atatamani
kurudi
gerezani kwa miaka mingine kumi
lakini haitawezekana tena!!!

Maoni 1 :

  1. CHUMA ULETE YA CHUNGU

    Kwanza CHUMA ulete Ni nini?
    Ni dawa ambayo utengenezwa kwa mkusanyiko wa utaratibu Fulani unaofanyika kwa pamoja kwa mlengo wa uvutaji au uvunaji wa fedha kutoka sehemu tofauti au mbalimbali.

    (Kwa uhitaji wa NDAGU AU JIHNI WA MALI AU FEDHA NA KINGA YA MWILI NA MALI KWA UJUMLA NIPIGIE SIMU MOJA KWA MOJA DOKTA MDIRO +255 742162843 KWA MAELEKEZO HATA KAMA UKIWA MBALI MALIPO NI BAADA YA MAFANIKIO).

    CHUMA ulete katika utengenezwaji hutumika jini anayeitwa GHUUL ambae uleta au uvuta fedha kimazingala kutoka sehemu mbalimbali kwa utaratibu maalumu. CHUMA ulete zipo Aina nyingi Ila leo nitazungumzia CHUMA ulete mdogo ya CHUNGU.

    Chuma uleteee ndogo ya chungu ambayoo inaluka na kwenda kukusanya pesa sehemu mbali mbali inavuta pesa ndanii .

    Hii chakula chake ni udi tuu na unaweza kunuwiza ukachagua ukaomba ikuletee pesa za aina gani wewe utachaguwa kama unavyoona hapo kwenye picha hii ni chuma uleteee ndogo mtu yeyotee anaweza kutengenezewa hata kama huna biashala pia hata Kama upo mbali kikubwa tu uwe na uwezo wa kutunza sili. Vile vileee hii inadumu miaka 5 itakubidii uludi kuja kutengeneza upya kafara ya damu ya kuku mwekunduu inatakiwa kila baada ya miezi 3.

    Tafuta chungu kama icho kwenye picha fanya duwa maalumu ambayo nitakupatia na tafuta udi Aina ya sain frola, metrofrolla au metromillan na kitambaa cheupe pia chumba kisafi kwa ajili ya ibada hiyo.

    Kumbuka hii ni chuma uleteee ndogo ya chungu hutakiwi kutoaa sili ya jini huyu na ufalume wa jini huyu maana utavunja miiko na maagano ya Jambo Hilo.

    Angalizo Piga simu kuepuka MATAPELI pia kwa maelekezo zaidi husifanye jambo hili bila maelekezo KAMILI.

    DOKTA MDIRO

    Call/whatsup +255 742162843

    JibuFuta